
Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Yohana 13:35.
Mtu aweza kuwa mtendakazi mwenza wa Mungu katika kutekeleza kazi kubwa ya ukombozi. Mungu humpatia kila mtu fursa yake ya kutenda baada ya kumpatia Neno lake kama mwongozo wa maisha yake. Pia amemtoa Roho Mtakatifu kama nguvu toshelevu kushinda mielekeo ya uovu ya kurithi na ile ya kujenga na kujenga tabia yake mwenyewe kwa wakala wa kibinadamu, na, kupitia kwake, na kwa wale wote watakaoingia katika anga zake za mvuto.
Wakala wa kibinadamu anahimizwa kushirikiana na Mungu, kudhihirisha rehema za Mungu, na wema wake, na upendo wake na hivyo kuwa na mvuto kwa watu wengine. Kila mtu anapaswa kuwa chombo ambacho Roho atakitumia kutenda kazi. Anaweza tu kuwa hivyo kwa kusalimisha akili zake zote kwa udhibiti wa Roho. Mungu alimtoa Roho wake siku ya Pentekoste na kupitia kwa Roho kutendakazi katika mioyo sikivu atawavuta wale wote ambao waumini watakutana nao.
Kupitia uhusiano wa kirafiki na kufahamiana na binadamu walio kama sisi, twaweza kuweka mvuto unaoinua moyo. Yesu anasema, “Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.” (Yohana 13:34).Upendo si jambo la mhemko wa ghafla, hisia ya kupitia, kutegemeana na mazingira; ni kanuni hai, nguvu ya kudumu. Nafsi inajazwa na mikondo ya upendo safi unaotiririka kutoka katika moyo ya Kristo, Chemchemi ambayo kamwe haikauki.
Ooh, ni kwa jinsi gani mioyo inahuishwa, ni kwa jinsi gani misukumo yake inaadilishwa, shauku zake kuongezwa, kwa mazungumzo haya! Chini ya elimu na uadibishwaji wa Roho Mtakatifu, wana wa Mungu hupendana wao kwa wao, kwa kweli, dhati na kwa unyofu,”haina fitina, haina unafiki.” (Yakobo 3:17).Na hii ni kwa sababu moyo unampenda Yesu. Upendo wetu sisi kwa sisi unatokana na sisi wote wawili kumpenda Mungu. Tu familia moja, tunapendana kama alivyotupenda. Unapolinganishwa na upendo huu wa kweli uliotakaswa na kubadilishwa, adabu ya juu juu ya kiulimwengu, maonesho yasiyo na maana ya upendo wa maneno vinakuwa kama makapi kwa ngano. -- Ellen G. White 1888 Materials, uk. 1508, 1509.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon