ROHO HUTUPATIA MANENO SAHIHI

Image may contain: text




Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.
Mathayo 10:20.

Miongoni mwa karama zote ambazo Mungu amempatia mwanadamu, hakuna yoyote ya thamani zaidi kuliko karama ya usemi, kama ikitakaswa kwa Roho Mtakatifu. Ni kwa ulimi ndipo tunasadikisha na kushawishi: kwa huo tunawasilisha sala na sifa kwa Mungu, na kwa huo tunaeleza mawazo ya pekee juu ya upendo wa Mkombozi. Wale ambao wamendaliwa kuelimisha akili za watu mara nyingi watakuwa na fursa za kusoma kutoka kwenye Biblia au vitabu vinavyofundisha kweli, na hivyo kuleta ushahidi kwa roho zilizoelimishwa.

Sauti ya Bwana inapoita ikisema, “Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?” Roho wa kiungu huweka jibu kwenye mioyo ili kuitikia, “Mimi hapa, nitume mimi” (Isaya 6:8). Lakini zingatia kwamba kaa la moto kutoka madhabahuni lazima kwanza liguse midomo yenu. Hapo ndipo maneno mtakayonena yatakuwa maneno ya busara na matakatifu. Hapo ndipo mtakuwa na hekima kujua lipi la kusema na lipi la kuacha bila kusema. Hamtajaribu kuonesha ustadi wenu kama wanateolojia. Mtakuwa makini kutoamsha roho ya ukinzani au kuchochea chuki, kwa kuingiza bila utaratibu vipengele vyote vya imani yetu. Mtapata mengi ya kuzungumzia ambayo hayataamsha upinzani, lakini ambayo yatafungua moyo kutamani maarifa ya kina zaidi ya Neno la Mungu.

Bwana anatamani mwe waongoaji wa roho; kwa hiyo, wakati ambapo hupaswi kuwalazimishia watu vipengele vya mafundisho ya imani, huna budi kuwa “tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu” (1 Petro 3:15). Hofu ya nini? Hofu ili vinginevyo maneno yako yasiwe na harufu ya kuonesha umuhimu binafsi, ili vinginevyo maneno yasiyokuwa na busara yasije yakazungumzwa, ili vinginevyo maneno na mwenendo visiwe vile visivyofanana na Kristo. Jifungamanishe na Kristo kwa uthabiti, kisha wasilisha neno la kweli kama lilivyo katika Yeye. Mioyo haiwezi kukosa kuguswa kwa kisa cha upatanisho.

Kadiri unavyojifunza upole na unyenyekevu wa Kristo, utajua kile upaswacho kuwaambia watu; kwani Roho Mtakatifu atakwambia maneno yapi ambayo huna budi kuzungumza. Wale wanaotambua umuhimu wa kudumisha moyo chini ya utawala wa Roho Mtakatifu watawezeshwa kupanda mbegu zitakazomea kwa ajili ya uzima wa milele. Hii ndiyo kazi ya mwenezaji wa injili.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.