KUGUSWA NA MOTO MTAKATIFU

Image may contain: bird, sky, text and outdoor






“Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”
(Luka 3:16).

Ilikuwa dhambi katika mfumo wa zamani kutolea dhahibu kwenye madhabahu isiyo sahihi, au kuruhusu uvumba ufukiziwe kwa kutumia moto mgeni. Tuko katika hatari ya kuchanganya mambo matakatifu na yale ya kawaida. Moto mtakatifu kutoka kwa Mungu hauna budi kutumiwa pamoja na matoleo yetu. Madhabahu halisi ni Kristo, na moto halisi ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anapaswa kuwavuvia, kuwafundisha, kuwasimamia na kuwaongoza wanadamu, na kuwafanya wawe washauri salama. Kama tukigeuka na kuwaacha wale waliochaguliwa na Mungu, tuko katika hatari ya kuuliza habari zetu kwa miungu migeni, na kutoa dhabihu kwenye madhabahu ya kigeni.

Mahubiri ya Neno yenye nguvu kuu zaidi hayatafaa kitu isipokuwa Roho akiwafundisha na kuwaangazia wale wanaosikiliza. Isipokuwa Roho akitenda kazi pamoja na kupitia wakala wa kibinadamu, roho hazitaokolewa wala tabia hazitabadilishwa kwa usomaji wa Maandiko. Mipango na ubunifu unaofanywa kwa ajili ya kazi haupaswi kuwa na mwonekano wa kuvutia usikivu wa watu kwenye nafsi. Neno ni nguvu, upanga mkononi mwa wakala wa kibinadamu. Lakini Roho Mtakatifu ndiye ufanisi wake, nguvu yake ya uhai katika kuigusa akili.

“Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu” (Yohana 6:45). Mungu ndiye asababishaye nuru iangaze mioyoni mwa wanadamu. Hivi ndugu zangu wanaohudumu watakumbuka kuwa ni muhimu kwamba Mungu atambuliwe kama chanzo cha nguvu yetu, na Roho atambuliwe kama Mfariji? Sababu inayomfanya Mungu atende kiasi kidogo hivyo kwa ajili yetu ni kwamba tunasahau kuwa wema halisi huja kupitia ushirikiano wetu na Roho Mtakatifu.

Daima Roho huionesha nafsi miguso ya mambo ya Mungu. Uwepo wa kiungu huonekana kuvinjari karibu, na kama akili ikiitikia, kama mlango wa moyo ukifunguliwa, Yesu hukaa pamoja na wakala huyo wa kibinadamu. Nguvu ya Roho inatenda kazi moyoni na kuongoza mwelekeo wa nia kuja kwa Yesu kwa imani hai na utegemezi kamili katika uwezo wa kiungu ili kutaka na kutenda kusudi Lake jema. Roho huyaamsha mambo ya Mungu, mara tu nafsi inapoamua na kutenda kulinga na nuru iliyodhihirishwa.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.