KUWA MAWAKALA WA MUNGU


Image may contain: sky, nature, text and outdoor




Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.
1 Wakorintho 3:5

Watumishi wa Mungu wote hawana karama zinazofanana, bali wote ni watendakazi wake. Kila mmoja anapaswa kujifunza kutoka kwa Mwalimu Mkuu, na kisha kuwasilisha kile alichojifunza. Wote hawatendi kazi moja ile ile, bali chini ya uwezo utakasao wa Roho Mtakatifu wote ni mawakala wa Mungu. Mungu anatumia karama mbalimbali katika kazi yake ya kujipatia roho [za watu] kutoka katika jeshi la Shetani.

“Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe” (1 Wakorintho 3:8). Mungu, na wala si mwanadamu, ni mhukumu wa kazi ya mwanadamu, na atagawa kwa kila mtu zawadi yake ya haki. Hajapewa mwanadamu ye yote jukumu la kuwahukumu watumishi mabalimbali wa Mungu. Bwana peke yake ndiye mhukumu na mtoa thawabu kwa kila kazi njema.

“Yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja” wanaojishughulisha na kazi ile ile-wokovu wa roho.

“Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu” (aya ya 9). Katika maneno haya kanisa linalinganishwa na shamba lililolimwa, ambalo ndani yake wakulima wanapaswa kufanya kazi, wakitunza mizabibu iliyopandwa na Bwana; na linalinganishwa na jengo, ambalo linapaswa kuwa hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. Kristo ni Mtendakazi Mkuu. Wote wanapaswa kufanya kazi chini ya usimamizi wake, wakimruhusu atende kwa ajili ya na kwa kupitia kwa wafanyakazi wake. Anawapa mbinu na stadi, na iwapo watayakubali maelekezo yake, atavisha kazi yao kwa mafanikio.

Hakuna hata mmoja anayepaswa kulalamika dhidi ya Mungu, ambaye amepanga kwa kila mtu kazi yake. Yeye ambaye ananung’unika na kuhangaika ambaye anataka kujiendea kama apendavyo, ambaye anatamani kuwaongoza [kuwanyoosha] watendakazi wenzake ili waendane na mawazo yake, huyo anahitaji mguso wa Mungu kabla hajawa na sifa za kutenda kazi yo yote. Kama hatabadilika, kwa hakika ataharibu kazi.

Kumbuka kuwa sisi ni watendakazi pamoja na Mungu. Mungu ndiye mtoa hoja mwenye nguvu zote na mwenye kuleta matokeo yanayotakiwa. Watumishi wake ni vyombo vyake.-Review and Herald, Dec. 11, 1900.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Latest
Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
Powered by Blogger.