
Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu. … Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
1 Kor. 12:1-6.
Vipaji vile ambavyo Kristo anavikabidhi kwa kanisa lake huwakilisha hasa karama na baraka ambazo zinatolewa na Roho Mtakatifu. “Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.” (1 Wakorintho 12:8-11).
Katika taratibu zote za Bwana, hakuna kitu kilicho kizuri kuliko mpango wake wa kuwapatia wanaume na wanawake karama mbalimbali. Kanisa ni bustani yake, ikiwa imepambwa kwa miti, mimea, na maua mbalimbali. Hategemei hisopo kujilinganisha na mwerezi, wala mzeituni kufikia kimo cha mtende adhimu. Wengi wamepokea mafunzo ya kiakili na kidini yaliyo finyu tu, lakini Mungu anayo kazi kwa ajili ya kundi hili kutenda, iwapo watafanya kazi kwa unyenyekevu, huku wakimtuainia yeye.
Vipawa mbalimbali vinatolewa kwa watu mbalimbali, ili watendakazi wapate kuhisi kila mmoja kumhitaji mwenzake. Mungu hutoa vipawa hivi, na vinatumika katika huduma yake, si kwa ajili ya kumtukuza mwenye navyo, si kwa ajili ya kumwuinua mwanadamu, bali kumwinua Mkombozi wa dunia. Vinapaswa kutumika kwa ajili ya faida ya wanadamu wote, kwa kuwakilisha ukweli, wala si kuthibitisha uwongo. … Katika kila neno na tendo, wema na upendo vitadhihirishwa; na kadiri kila mtendakazi anavyojaza kwa uaminifu sehemu yake iliyopangwa, ombi la Kristo kwa ajili ya umoja wa wafuasi wake litajibiwa, na dunia itafahamu kuwa hawa ni wanafunzi wake. - Signs of the Times, March 15, 1910.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon