AKIJA MARA YA PILI

Image may contain: text





"Kwa maana sisi, wwnyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake."
Wafilipi 3:20,21

Utukufu wa ubinadamu wa Kristo haukuonekana alipokuwa hapa duniani. . . . Ubinadamu ule ule utaonekana akishuka kutoka mbinguni, akiwa amevishwa utukufu, akiwa mshindi, akiwa ametukuzwa.

Kristo atakuja katika utukufu wake mwenyewe, katika utukufu wa Baba yake, na katika utukufu wa malaika watakatifu. Malaika elfu Kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, ambao ni wana wa Mungu wazuri, wenye upendo uliozidi na utukufu, watamsindikiza njiani mwake. Mahali pa taji ya miiba, atakuwa amevaa taji ya utukufu - taji ndani ya taji. Mahali pa vazi kuukuu la kahawia, atakuwa amevishwa vazi lililo jeupe sana, "jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe" (Mk 9:3). Na kwenye vazi lake na paja lake jina litakuwa limeandikwa, "MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA." Uf. 19:16.

Mbinguni kote hakutakuwa na malaika, wakati watakatifu watakapokuwa wakimtazamia na kutazama mbinguni, kama walivyokuwa watu wa Galilaya pale alipopaa kutoka katika mlima wa Mizeituni. Ndipo wale tu walio watakatifu, wale ambao wamemfuata kikamilifu yeye aliye Kielelezo cha utiifu, watasema kwa shangwe na shauku huku wakimtazama, "Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie." Nao watabadilishwa "Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho" - parapanda ambayo itawaamsha watakatifu waliolala na kuwaita watoke mavumbini, wakiwa wamevishwa hali ya utukufu ya kutokufa, huku wakipaza sauti, "Ushindi! Ushindi dhidi ya mauti na kaburi!"
(Maranatha, uk. 282)

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.