
Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli. Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Yohana 17:18-20.
Baba yangu wa Mbinguni, naja kwako wakati huu, kama nilivyo, maskini na mhitaji, nikikutegemea wewe. Nakuomba unipe na uwape watu hawa neema inayojenga tabia kamilifu ya Kikristo. Je, hutawahurumia watu hawa? Hebu nuru yako na iangaze ndani ya nia zao, na katika hekalu la roho. Mwokozi wangu, Wewe umetoa maisha yako kununua urithi Wako, ili, kama washindi, wapate kuingia katika ufalme wa Mungu, ambapo hawatatoka tena milele. Wabariki wale ambao wameonyesha shauku yao ya kukutumikia. Wajaze kwa Roho wako.
Nakuomba, Baba wa Mbinguni, uruhusu Roho wako Mtakatifu aje kwa watu hawa. Hebu wokovu wako ufunuliwe. Gusa mioyo yao, ukawafanye kuwa wapole. Walainishe kwa Roho wako Mtakatifu, wasaidie kuona kazi inayopaswa kufanywa kwa ajili ya jirani zao, na kwa roho zinazoangamia kote kuwazunguka. Wape kuyatambua majukumu yao! Hebu wafue mavazi ya tabia zao, na kuyafanya meupe katika damu ya mwana kondoo. Je hutawazingira kwa mikono yako ya rehema? Wasihi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ili wajaribu kutumia nuru yao kutangaza kwa wale ambao bado hawajajua ukweli. Lielekeze kanisa lako Bwana, ili watende kazi kwa ajili ya roho.
Mwokozi wangu, jifunue kwa watu hawa. Hebu upendo wako ukadhihirike. Hebu na ufunuliwe! Washike watu wako, ili shetani asiwe na nafasi ya kuleta mapenzi na njia yake kwao. Wasaidie kupenya katika vipingamizi vyote, ili hatimaye waweke taji zao katika miguu ya Yesu, kwenye mji wa Mungu; na utukufu wote utaliendea jina lako. Amina. -- Review and Herald, July 16, 1908.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon