HAKUNA MUDA WA KUPOTEZA

Image may contain: text




Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka. Yeremia 8:20.

Bwana anakuja. Historia ya dunia karibia itafungwa. Je uko tayari kukutana na mhukumu wa dunia? Kumbuka “hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu” (Yakobo 2:13). Litakuwa jambo la kutisha kiasi gani katika siku ile kuu ya mwisho kugundua kwamba wale ambao tulifahamiana na kushirikiana nao kwa karibu wametengwa mbali nasi milele; kuona wanafamilia yetu, huenda watoto wetu, kuwa hawakuokolewa; kugundua kuwa wale waliowahi kututembelea nyumbani, na kula nasi mezani, wako miongoni mwa waliopotea. Kisha tutajiuliza swali, je hii ilitokana na kushindwa kwangu kuvumilia, tabia yangu ambayo haikufanana na Kristo; je ni kwa sababu sikujitawala nafsi, ndio maana dini ya Kristo haikuwa na mvuto kwao?

Sharti ulimwengu uonywe juu ya ujio wa Bwana uliokaribia. Tumebakiza muda kidogo tu wa kufanya kazi. Miaka imepita milele ambayo ingetumika vyema kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na kwa kusambaza ukweli kwa wengine. Mungu anawataka watu wake walio na nuru kubwa, ambao kazi kubwa imewekwa juu yao, na kuwa thabiti katika ile kweli, kwamba sasa wafanye kazi kwa ajili yao wenyewe na wengine kuliko walivyowahi kufanya. Tumia kila kipaji; weka kila stadi katika vitendo, kila talanta uliyokirimiwa, tumia nuru yote aliyokupatia Mungu kuwatendea wengine mema. Msijaribu kuwa wahubiri; bali iweni watumishi wa Mungu.

Kadiri ukweli unavyoeleweka vyema kwa watendakazi, ndivyo utakavyoonekana kwa nuru ya ajabu; kadiri unavyojitahidi kuwapa nuru wengine, huku nia yako ikiwa chini ya uwezo wa Roho wa Mungu, fikra zako zitaelekezwa kwa vitu vile vyenye maslahi ya milele. Katika jitihada za namna hiyo, zikichanganywa na maombi kwa ajili ya kupata nuru ya kiungu, moyo wako mwenyewe utadunda kwa nguvu ihuishayo ya neema ya Mungu; matakwa yako mwenyewe yatang’aa kwa hisia ya kiungu, na maisha yako yote ya Kikristo yatakuwa ya uhalisia zaidi, bidii zaidi, na ya maombi zaidi. Hivyo kwa Kristo kukaa moyoni mwako, waweza kuwa mtendakazi pamoja na Mungu. --Home Missionary, Feb. 1, 1898.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.