MAWAKALA WA MBINGUNI WANATUNGOJA

Image may contain: sky, text, nature and outdoor





Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Warumi 10:9,10.

Mungu anataka kila talanta na uwezo vitumike. Wakati lawama juu ya uvivu na uzembe itakapokuwa imeondolewa kabisa kanisani, Roho wa Mungu atadhihirishwa kwa uzuri; uwezo wa kiungu utaunganika na jitihada za kibinadamu, kanisa litaona majaaliwa ya uingiliaji kati wa Bwana wa Majeshi, nuru ya kweli itasambaa, ukweli wa Mungu na wa Yesu Kristo aliyemtuma. Kama ilivyokuwa nyakati za mitume, roho nyingi zitamgeukia Bwana. Dunia itaangazwa kwa utukufu wa malaika kutoka mbinguni.

Ili ulimwengu usadikishwe juu ya dhambi kama waasi wa sheria ya Mungu, wakala lazima awe Roho Mtakatifu akitenda kazi kupitia vyombo vya kibinadamu. Sharti kanisa sasa liondoe usingizi wake unaofanana na kifo; kwani Bwana anangoja kubariki watu wake ambao watatambua mbaraka utakapowajia, na kusambaza katika miali ya nuru bayana yenye nguvu. “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote... Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu” (Ezekieli 36:25-27).

Ili hali ya jangwa ya kanisa ipate kugeuka kuwa shamba linalozaa, na shamba linalozaa liwe msitu, basi yapasa Roho Mtakatifu wa Mungu amwagwe kwa watu wake. Kwa muda mrefu sasa mawakala wa kimbingu wanawangoja mawakala wa kibinadamu, washiriki wa kanisa, kushirikiana nao katika kazi kubwa inayopaswa kufanywa. Wanakungoja. Shamba ni kubwa mno, mpango umepangwa kwa namna ya kitaalamu sana, ili kila moyo uliotakaswa uingine katika huduma ya wakala ya uwezo wa kiungu . . . .

Hebu wote wanaouamini ukweli wa wakati huu waweke kando tofauti zao; waweke kando wivu, na masengenyo, na mawazo maovu. Shikamaneni, shikamaneni. “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo” (1 Petro 1:22). -- General Conference Bulletin, Feb. 28, 1893.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.