
Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. 2 Wakorintho 5:19.
Katika kazi ya kuwaokoa wanadamu, wanadamu na malaika wanapaswa kufanya kazi kwa upatanifu, wakifundisha ukweli wa Mungu kwa wale wasioujua, ili wapate kuwekwa huru toka vifungo vya dhambi. Ukweli pekee unaweza kuwaweka wanadamu huru. Uhuru upatikanao kutokana na kuijua kweli unapaswa kutangazwa kwa kila kiumbe. Baba yetu wa mbinguni, Yesu Kristo, na malaika wa mbinguni wote wanapenda kazi hii kuu na takatifu.
Mwanadamu amepewa fadhila ya juu ya kufunua tabia ya Mungu kwa kuhangaika bila ubinafsi kuokoa mwanadamu toka katika shimo la uharibifu ambalo ametumbukia. Kila mwanadamu atakayejitoa ili aelimishwe na Roho Mtakatifu anapaswa kutumika kukamilisha kusudi hili la kimbingu. Kristo ni kichwa cha Kanisa lake, na litamtukuza zaidi pale kila nyanja ya kanisa itakaposhiriki katika kazi ya kuokoa roho.. . . .
Kuna furaha kubwa zaidi mbinguni kwa ajili ya mdhambi mmoja atubuye, kuliko kwa watu tisini na tisa ambao wanadhani hawana haja ya kutubu. Tunaposikia juu ya mafanikio ya ukweli mahali popote, hebu kanisa lote lishiriki kwa kuimba nyimbo za shangwe, hebu sifa ziinuliwe kwa Mungu. Hebu tulihimidi jina la Mungu, nasi tutajazwa ari zaidi ya kuwa watendakazi pamoja na Mungu. Mungu anatutaka tutimize agizo”Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15).Lakini yatupasa tuache nafasi ya kutosha kwa ajili ya utendaji wa Roho Mtakatifu, ili kwamba watendakazi wapate kufungamanishwa pamoja ili wasonge mbele katika nguvu ya kikosi kilichoshikamana cha askari.
Hebu wote wakumbuke kwamba”tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu.” (1 Wakorintho 4:9). Hivyo kila mmoja na aulize kwa unyenyekevu na kicho, eneo langu la kazi ni lipi? Kujiweka wakfu kikamilifu kwa kazi ya Mungu kutafunua mvuto unaobadilisha wa Roho Mtakatifu katika kila hatua yetu safarini.--Review and Herald, July 16, 1895.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon