
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini.
Rum 13:11.
Ndugu zangu, unapaswa kumtawaza Yesu moyoni, na ubinafsi lazima ufe. Sharti tubatizwe na Roho Mtakatifu, na kisha hatutaketi chini, tukisema kwa kutojali, “Liwalo litakuwa; sharti unabii utimie.” Amka, nakusihi, amka! Kwani umebeba majukumu matakatifu mno. Kama walinzi waaminifu, unapaswa uone upanga ukija, na kutoa maonyo, ili wanaume na wanawake wasitende kipumbavu yale ambayo wangeyaepuka kama tu wangejua ukweli. Bwana ametupatia nuru juu ya kile kinachoujia ulimwengu ili tuwajulishe wengine, na hatutakosa kuwa na hatia ikiwa tutaridhika kukaa kimya, tukikunja mikono, na kukwepa suala la msingi kwa kujali mambo yenye umuhimu wa chini. Nia za wengi zimejaa ushindani, nao wameikataa nuru iliyotolewa kwa njia ya shuhuda, kwa sababu haikuendana na mitazamo yao.
Mungu hamlazimishi yeyote kufanya kazi yake. Kila mtu na aamue mwenyewe kwamba atachagua kuuangukia mwamba na kuvunjika vunjika au la. Mbingu zinashangaa kuona ujinga unaotawala. Wewe binafsi unahitaji kufungua moyo wako wenye kiburi kwa Roho wa Mungu, unahitaji kuhakikisha kuwa uwezo wako wa kiakili unatakaswa kwa ajili ya kutenda kazi ya Mungu. Uwezo wa Mungu ubadilishao yapaswa uwe juu yako, ili nia yako ipate kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu, ili uwe na nia ile iliyokuwa ndani ya Kristo.
Kama walinzi wakileweshwa na dawa ya usingizi ya shetani na kushindwa kutambua sauti ya Mchungaji wa kweli, na kutopokea maonyo, nakuambia kwa kicho cha Mungu, damu ya roho hizo itadaiwa kwao. Walinzi sharti wawe macho kabisa, watu ambao hawatasinzia katika malindo yao, usiku au mchana. Lazima wapige mlio fulani wa baragumu, ili watu waache uovu, na kuchagua wema. Ujinga na kutojihusisha kizembe haviwezi kukubalika kuendelea. Kote kutuzunguka kuna washambuliaji na vipande vya mawe vilivyofichika ambavyo vitakata migongo yetu vipande vipande, na kutuachia majereha makubwa tusiyoweza kuyamudu, isipokuwa kama tutamfanya Mungu kimbilio na msaada wetu. -- Review and Herald, Dec. 24, 1889.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon