KUFUATA MAAGIZO YA NAHODHA


Image may contain: text



Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
2 Timotheo 2:3, 4.

Tuna muda mfupi tu wa kuendelea na mapambano; kisha Kristo atakuja, na mandhari hii ya uasi itafungwa. Ndipo jitihada zetu za mwisho zitakuwa zimefanywa za kutendakazi na Kristo katika kuendeleza ufalme wake. Baadhi ambao wamesimama mstari wa mbele wa vita, kwa jitihada kubwa wakiupinga uovu ujao, wanaanguka katika mahali pa kazi; wengine wanatazama kwa huzuni mashujaa wakianguka, lakini hawana muda wa kukomesha kazi. Yawapasa kushikamana, wapokee bendera toka mikononi mwa wale waliokumbwa na kifo, na kwa nguvu mpya wauthibitishe ukweli na heshima ya Kristo. Kuliko ilivyowahi kuwa, upinzani sharti uwekwe dhidi ya dhambi --- dhidi ya nguvu za giza. Muda unataka jitihada za nguvu na za kudhamiria kwa upande wa wale wanaouamini ukweli wa leo. Yawapasa wafundishe kweli kwa maagizo na kielelezo.

Kama muda unaonekana mrefu mno kwetu kumsubiri mwokozi wetu, kama, kwa kunyenyekeshwa na mateso na kuchakazwa na kazi ya taabu, tunajisikia kushindwa kuvumilia hadi utume wetu ukamilike, ili tutoke vitani kwa heshima, hebu tukumbuke – na hebu hiyo kumbukumbu izuie kila nung’uniko – kwamba Mungu anatuacha duniani kukabili dhoruba na migogoro, kukamilisha tabia ya Kikristo, kuwa na ujuzi bora zaidi juu ya Mungu Baba yetu na Kristo Kaka yetu Mkubwa, na kumtendea kazi Bwana wetu ya kuleta roho nyingi kwa Kristo, ili kwa mioyo ya furaha tusikie maneno: “Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.”(Mathayo 25:21).

Uwe mvumilivu, askari wa Kikristo. Bado kitambo kidogo, na Yeye ajaye atakuja. Usiku wa uchovu wa kungoja, na kukesha, na kuomboleza unakaribia kuisha. Muda si mrefu thawabu itatolewa; siku ya milele itapambazuka. Hakuna muda wa kulala sasa -- hakuna muda wa kujihusisha na mambo ya kusikitisha yasiyo na manufaa. Yeye anayediriki kusinzia sasa hivi atakosa fursa za thamani za kutenda mema. Tumepata fadhila yenye heri ya kukusanya miganda katika mavuno makuu; na kila roho iliyookolewa itakuwa nyongeza ya nyota katika taji ya Yesu, Mwokozi wetu anayeheshimika sana. Ni nani mwenye hamu ya kuweka kando silaha, wakati ambapo kwa kuendelea na vita kwa kitambo kidogo atapata tunu mpya milele zote? -- Review and Herald, Oct. 25, 1881.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.