KUDUMU KUMTEGEMEA MUNGU KIKAMILIFU

Image may contain: ocean, shoes and text





Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi.
1Kor 2:1-3.

Kutakuwapo nyakati ambapo kanisa litaamshwa kwa nguvu ya kiungu, na matokeo yake yatakuwa kutenda kazi kwa bidii; kwani nguvu ya Roho Mtakatifu iletayo uzima itawapa msukumo washiriki wake kutoka na kwenda kuleta roho kwa Kristo. Lakini wakati shughuli hii itakapodhihirika, wale watendao kazi kwa bidii kabisa watakuwa salama tu kwa kumtegemea Mungu daima na kwa njia ya maombi ya bidii yasiyokoma. Itawabidi kuomba kwa bidii kwa njia ya neema ya Kristo ili waepushwe na kutopanda kiburi kutokana na kazi yao, au kuigeuza iwe ndiyo mwokozi wao. Yawapasa wadumu kumwangalia Yesu, ili watambue kwamba ni uwezo wake unaotenda kazi, na hivyo waweza kuelekeza utukufu wote kwa Mungu.

Tutahitajika kufanya jitihada za dhati kupanua kazi ya Mungu, na maombi kwa Baba yetu wa mbinguni yatakuwa ya muhimu sana. Litakuwa jambo la muhimu kuingia katika maombi kwenye chumba cha faragha, katika familia, na kanisani. Kaya zetu sharti ziwekwe katika utaratibu, na jitihada kubwa zifanywe kumjengea kila mwana familia hamu ya kufanya shughuli ya umishenari. Ni lazima tufanye jitihada za kutumia huruma za watoto wetu katika kazi ya bidii kwa ajili ya wale ambao hawajaokolewa ili wakati wote wafanye kila wawezalo mahali pote kumwakilisha Kristo.

Lakini tusisahau kwamba kadri shughuli zinavyoongezeka, nasi tunafanikiwa kufanya kazi ambayo inapaswa kukamilishwa, kuna hatari ya kutumainia mipango na mbinu za kibinadamu. Kutakuwa na mwelekeo wa kuomba kidogo, na kuwa na imani kidogo. Tutakuwa katika hatari ya kupoteza utambuzi wetu wa kumtegemea Mungu, ambaye pekee aweza kuifanikisha kazi yetu; Lakini ingawa huo ndio mwelekeo, hebu tusidhani ya kuwa sehemu ya mwanadamu anayotakiwa kufanya ni kidogo. La hasha! Hapaswi kufanya kidogo, bali kufanya zaidi kwa kupokea kipawa cha mbinguni, Roho Mtakatifu. Ulimwengu kwa hekima yake wenyewe haukumjua Mungu, na kila nguvu ya kibinadamu kiasilia, kwa kiwango kidogo au kikubwa, inapingana na Mungu. Imetupasa kumwangalia Yesu, na kushirikiana na wakala wa kimbingu, kupeleka maombi yetu kwa Baba katika jina la Yesu. --Review and Herald, July 4, 1893.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

K
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.