
Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Luka 11:13.
Ahadi ya kipawa cha Roho Mtakatifu haieleweki kama ipasavyo; fadhila zitakazopatikana kutokana na kupokea kipawa hicho hazitambuliwi ipasavyo. Mungu anataka kwamba kanisa lake lidai ahadi zake kwa imani, na kuomba uwezo wa Roho Mtakatifu uwasaidie kila mahali. Anatuhakikishia kuwa yuko tayari kabisa kuwapatia Roho Mtakatifu wale wanaomwomba, kuliko wazazi walivyo tayari kuwapa zawadi watoto wao. Kwa vile inawezekana kwa kila mtu kupata upako wa mafuta wa mbinguni, “wala hamna haja ya mtu kuwafundisha;” (1 Yn. 2:27), na hakuna udhuru wa kukimbia majukumu; hakuna zamu inayopaswa kutokubalika, hakuna wajibu wa kukwepwa. Kristo mwenyewe ndiye nguvu ihuishayo, akitenda kazi ndani ya kila askari na kupatia kila askari kwa wakala wa Roho Mtakatifu. Ufanisi wa Roho wa Mungu utafanya kazi za wote walio radhi kujisalimisha kwa uongozi wake ziwe na manufaa.
Mungu anazungumza na kila nia iliyo tayari kupokea nguvu ya Roho wake Mtakatifu. Anatuma wajumbe ili wakatoe ujumbe wa onyo kwa kila mahali. Mungu anapima kujitoa kwa makanisa yake, na utayari wao kuonesha utii kwa uongozi wa Roho. Maarifa yataongezwa. Wajumbe wa mbinguni wataonekana wakienda huku na huko, wakitumia kila njia iwezekanayo kuwaonya watu juu ya hukumu ijayo, na kuwapatia habari njema za wokovu kupitia kwa Bwana Yesu Kristo. Viwango vya haki vitapaswa kuinuliwa.
Roho wa Mungu anashawishi mioyo ya watu, na wale wanaoitikia ushawishi wake watafanyika nuru ya ulimwengu. Kila mahali wanaonekana wakienda kutangaza kwa watu wengine nuru waliyoipokea, kama walivyofanya baada ya Roho Mtakatifu kushuka katika siku ya Pentekoste. Na kadri wanavyoangaza kwa nuru yao wanapokea nguvu nyingi zaidi za Roho. Dunia inaangazwa kwa utukufu wa Mungu. -- Australasian Union Conference Record, Apr. 1, 1898.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon