
Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
2 Kor. 12:10.
Kumekuwepo hata hivyo wengi mno wanaojiangalia majaribu na matatizo yao wenyewe. Bali wanaposahau nafsi zao wenyewe, na kutazama shida ambazo zinawataabisha wengine, hawatakuwa na muda kukuza shida zao wenyewe. Kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Bwana ni hati ya dawa kwa maradhi ya nia, na mkono wa msaada kuondoa mizigo ambayo Kristo amebeba kwani wote walio urithi wake watapunguza mizigo yetu, wala hawataonekana wenye kustahili kutajwa. Kazi ya kweli na dhati itajenga afya ya nia kwa kujenga afya ya misuli.
Ni ile hali ya kudumu kutengeneza magonjwa na mizigo ndiyo inaua. Tunapaswa kuridhika kubeba uchovu wa majukumu yetu ya kila siku; na mlemeo mkubwa wa madeni ya kesho—yaache haya mahangaiko yote hadi muda wake ufike.
Tumeitwa sasa ili tuelimishwe, ili tupate kutenda kazi ambayo Mungu ametupatia, wala haitayaseta maisha yetu.Mtu wa hali ya chini kabisa anaweza kuwa na sehemu katika kazi, na sehemu katika tunu wakati kutawazwa kutakapofanyika, na Kristo, Mwombezi na Mkombozi wetu, atakapokuwa Mfalme wa wale aliowakomboa.
Yatupasa sasa kufanya kila tuwezalo kuyaweka maisha yetu binafsi wakfu kwa Mungu. Si watu wakuu zaidi, au wenye talanta zaidi, au wenye elimu zaidi, ambao tunawahitaji katika kuwasilisha ukweli wa wakati huu; bali watu wanaomjua Mungu na Yesu Kristo, ambaye amemtuma.
Uchaji Mungu wa mtu binafsi utamstahilisha mtendakazi yeyote, kwani Roho Mtakatifu anatawala ndani yake, na ukweli wa wakati huu unakuwa nguvu, kwa vile mawazo na matendo yake ya kila siku yanaendana na Kristo.
Kristo anakaa ndani yake; na nafsi ya hali ya chini sana iliyounganishwa na Kristo, ni nguvu na kazi yake itadumu. Bwana atusaidie kuelewa mapenzi yake ya kiungu, na kuyatenda kwa moyo, bila kuyumbishwa, na kutakuwa na furaha katika Bwana.--Home Missionary, Nov. 1, 1897.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
EmoticonEmoticon