
“Nawe utasema naye, na kuyatia maneno kinywani mwake; nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na pamoja na kinywa chake, na kuwafundisheni mtakayofanya.” (Kutoka 4:15).
Mtu aliye mtendakazi pamoja na Kristo anapofikisha mahali pake neno la kweli moyoni mwa mdhambi kwa unyenyekevu na upendo, sauti ya upendo huzungumza kupitia wakala huyo wa kibinadamu. Wenye maarifa wa mbinguni hufanya kazi pamoja na wakala mwanadamu aliyejiweka wakfu, na Roho hutenda kazi rohoni mwa asiyeamini. Ufanisi wa kuamini hutoka kwa Mungu na kuingia moyoni mwa mtu huyo, na mdhambi hupokea ushahidi wa Neno la Mungu.
Kupitia nguvu ya neema ya Roho Mtakatifu hubadilishwa na kuwa mmoja na Kristo katika nia na kusudi. Upendo wake kwa Mungu huongezeka, huwa na njaa ya kupata uadilifu na hutamani kufanana zaidi na Bwana wake. Kwa kumtazama Kristo, anabadilishwa toka utukufu hadi utukufu, toka tabia moja hadi nyingine, na hufanana na Yesu zaidi na zaidi. Hujazwa upendo kwa ajili ya Kristo na hujazwa upendo wa kina usiotulia kwa ajili ya roho zinazoangamia, Naye Kristo hufanyika ndani yake tumaini la utukufu. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12).
Tunahitaji zaidi utendaji wa yule asiye na ukomo na kuwatumainia mawakala wanadamu kwa kiasi kidogo sana. Hatuna budi kuwaandaa watu kusimama katika siku aliyoiandaa Mungu; tunapaswa kuvuta mawazo ya watu kwenye msalaba wa Kalvari, kubainisha wazi sababu iliyomfanya Kristo atoe kafara kuu kiasi hicho. Tunapaswa kuwaambia wanadamu kwamba wanaweza kurejea kwenye uaminifu wao kwa Mungu na katika utii wao wa amri Zake. Mdhambi anapomwangalia Kristo kama mpatanishi wa dhambi zake, hebu wanadamu wakae pembeni. Hebu wamtangazie mdhambi kwamba Kristo “ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote” 1Yohana 2:2
Mtie moyo atafute hekima kutoka kwa Mungu; kwa sababu kupitia maombi ya dhati atajifunza njia ya Bwana kwa ukamilifu zaidi kuliko kama akielekezwa na mshauri fulani aliye mwanadamu. Ataona kwamba ulikuwa uvunjaji wa sheria ndio uliosababisha mauti ya Mwana wa Mungu asiye na ukomo, naye atachukia dhambi zilizomwumiza Yesu. Kadiri anavyomwangalia Kristo kama Kuhani Mkuu mwenye huruma na mpole, moyo wake utahifadhiwa katika majuto.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
1 comments:
Write commentsTitan Metal Studio is coming to NieR Games
ReplyIn fact, this is one of black titanium rings the first things burnt titanium you ever did sunscreen with titanium dioxide with NieR aftershokz titanium games on titanium dive watch your gaming For starters, the
EmoticonEmoticon