1. Wakati Waimbaji wa zamani walipomaliza kuimba, Waabuduo walitokwa na Machozi kwa sababu waliimba kwa Utukufu. Lakini sasa hivi baada ya akina Delila na Yezebeli kuimba Washiriki wanawapigia Makofi kuwapatia Waimbaji Utukufu.
2. Zamani Hubiri lilipotolewa Washiriki walilia na walijutia dhambi zao, lakini leo wakati Hubiri linaendelea Watu hutoa Pesa, hupiga Miruzi na kupiga kelele za ushabiki.
3. Zamani walienda Kanisani na Ujumbe uliwapatia Waumini Imani lakini leo Watu huenda Kanisani na Waumini hupatiwa Vitu vya uongo kama vile Mafuta ya Mzeituni, Leso, Vazi jeupe, Lebo, Maji matakatifu na Kalenda za Bahati njema.
4. Watu wa zamani walibeba Biblia zao kwa kuwa hawakumuonea Yesu aibu lakini baadhi yetu leo wanabeba Ipad Kanisani kwa kuwa wanaona aibu kuonekana ni Watu wa Yesu na kwa hao Yesu atawaonea aibu Siku ya mwisho.
5. Wenye nia kama ya zamani huenda Kanisani wakiwa wamezifunika vizuri Nywele zao lakini wa sasa wanafunika Nywele zao kwa Mawigi ya Brazili.
6. Wakati wa Maombi wa zamani hufumba Macho yao na kumpa Mungu usikivu wao wote lakini wa sasa hufumbua Macho yao na kuangalia huku na huko kama Majambazi yenye Silaha na hata hupokea Simu wakati wa Maombi.
7. Wa zamani hunesanesa kwa Utukufu wakiwa na Shukurani na Sadaka lakini wa sasa haogopi hata kucheza Muziki wa Doro, Awilo na Azonto kibwetani.
8. Wa zamani huenda Kanisani wakiwa wamefunika Miili yao na hujali sana uzuri wa ndani lakini wa sasa huvaa Sketi fupi, huonesha kila kitu na kila kitu hakina uhalisia na huonekana kama Jini. Ni rahisi sana kwao kuanguka kwa kuwa kila alichovaa kinavutia Mashetani.
9. Zamani Wadhambi walienda Nyumbani wakilia leo Wadhambi hurudi Nyumbani wakifurahia.
10. Wa zamani waliitikia Wito Machozi yakitiririka katika Nyuso zao, wa sasa wanatafuna Bazoka wakati wa Wito. Ooh Bwana iamshe Kazi yako. Tunaomba utuamshe kabla ya ujio wako.
Bwana akubariki

EmoticonEmoticon