OMBI LA MAMA MWENYE UPENDO



Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
Ufunuo 3:21.

Kupitia kwa mama yao, Yakobo na Yohana waliwasilisha ombi kwamba wapewe ruhusa ya kuchukua nafasi za juu kabisa za heshima kwenye ufalme wa Kristo. Licha ya maelekezo ya Kristo aliyoyatoa kwa kurudia rudia juu ya aina ya ufalme wake, wanafunzi hawa vijana bado walipendezwa na tumaini la Masihi ambaye atachukua kiti cha enzi na mamlaka ya kifalme kulingana na tamaa za watu…

Lakini Mwokozi alijibu, “Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?” Walikumbuka maneno yake ya mafumbo yaliyoelekeza kwenye jaribu na mateso, hata hivyo walijibu kwa ujasiri, “Twaweza.” Waliona kuwa ni heshima kubwa kuthibitisha utii wao kwa kushiriki yote ambayo yangemwangukia Bwana wao.

Kristo akatamka, “Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa,”… Yakobo na Yohana walikuwa wawe washirika pamoja na Bwana wao katika mateso – mmoja, hatima yake ikiwa kifo kilichokuwa kinakuja upesi kwa upanga; mwingine, kati ya wanafunzi wake ambaye angemfuata Bwana wake kwa muda mrefu zaidi ya wanafunzi wengine wote katika kufanya kazi na kuaibishwa pamoja na mateso.

Kisha akaendelea, “Lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.”… Kwenye ufalme wa Mungu, mtu hapewi cheo kwa upendeleo. Cheo hakifanyiwi kazi, wala hakipokelewi kutokana na kutolewa kiholela. Ni matokeo ya tabia. Taji na kiti cha enzi ni ishara za hali ambayo mtu anaipata – ishara za ushindi wa nafsi kupitia kwa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo…

Yeye atakayesimama karibu kabisa na Kristo atakuwa yule ambaye amekunywa kwa ndani kabisa roho yake ya upendo unaofanya nafsi ijitoe – upendo ambao “hautakabari; haujivuni;… hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya,” – upendo ambao unamsukuma mwanafunzi, kama ulivyomsukuma Bwana wetu, kutoa vyote, kuishi na kutenda na kutoa hata kufa, kwa ajili ya kuokoa binadamu.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.