Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Luka 22:31, 32.
Akiwa ni jasiri, mshari, mwenye kujiamini, mwepesi kuelewa na aliye mbele katika kutenda, mwenye haraka katika kulipiza kisasi wakati huo huo mwepesi kusamehe, Petro mara kwa mara alikosea na vivyo hivyo alikemewa. Wala utii wake wa moyo na kujitoa kwake kwa Kristo havikupungua katika kuonekana na pia kupongezwa.
Kwa uvumilivu, kwa upendo ulioona tofauti, Mwokozi alishughulika na mwanafunzi wake aliyekuwa na harara, akijaribu kudhibiti hali yake ya kujiamini nafsi na kumfundisha unyenyekevu, utii na kutumaini. Lakini fundisho hili alilipata kwa sehemu tu…. Kwa kurudia rudia onyo lilitolewa, wewe “utanikana mara tatu ya kuwa hunijui.”
Ilikuwa ni roho hii iliyohuzunishwa, yenye upendo ya mwanafunzi ambayo ilinena kwa kuapiza, “Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni.”.. Wakati pale kwenye ukumbi wa hukumu maneno ya kukana yalipotamkwa; wakati upendo na utii wa Petro viliamshwa kutokana na kutupiwa jicho na Mwokozi la huruma na upendo na huzuni, vilimfanya aende kwenye bustani ambapo Kristo alilia na kuomba; wakati matone ya machozi yake ya majuto yalipodondoka kwenye upanga ambao ulikuwa na unyevu wa matone ya damu ya maumivu yake – ndipo maneno ya Mwokozi, “Nimekuombea wewe”…yalibaki moyoni mwake.
Kristo, japo aliona dhambi yake, hakuwa amemwacha akate tamaa. Kama lile jicho ambalo Yesu alimtupia lilitamka hukumu badala ya huruma; ikiwa kwa kutaja dhambi kabla alikuwa ameshindwa kuzungumzia tumaini, giza lililofunika Petro lingekuwa nene kiasi gani!...
Yeye ambaye hakumwacha mwanafunzi wake asipitie maumivu, hakumwacha peke yake katika uchungu. Upendo wake haushindwi na wala hauachi. Wanadamu, ambao wao wenyewe wamo katika uovu, wanao mwelekeo wa kutoshughulika kwa upendo na huruma na wanaojaribiwa na wakosaji. Hawawezi kusoma moyo, hawajui mapambano na maumivu yake.
Wanalo hitaji la kujifunza juu ya kemeo ambalo ni upendo, juu ya pigo linalojeruhi ili liponye, juu ya onyo linalonena tumaini…. Muujiza wa wema wa Mungu ndio uliokuwa badiliko la Petro. Ni fundisho la maisha kwa wote wanaotaka kufuata nyayo za Mwalimu Mkuu.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon