CHINI YA NGUVU YA SHETANI



Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Mathayo 16:23.

Daima Shetani anajiingiza kati ya nafsi ya mtu na Mungu…Kulingana na kilichompata Petro, hili ni fundisho ambalo yapasa lijifunzwe kwa uangalifu.

Petro hakutamani kuona msalaba katika kazi ya Kristo. Mguso ambao maneno yake yaliweka, ulikuwa kinyume kabisa na kile ambacho Kristo alitamani kuuweka kwenye akili za wafuasi wake, na Mwokozi alisukumwa kutoa moja ya kauli kali sana za kukemea ambazo zilipata kutoka kwenye midomo yake…

Shetani alikuwa akijaribu kumkatisha tamaa Yesu na kumtoa katika utume wake; naye Petro, katika mapenzi ya kijinga, alikubali kuwa sauti ya lile jaribu. Mfalme wa uovu alikuwa ndiye chanzo cha wazo lile. Uchochezi wake ndio uliokuwa chanzo ule wito wa harara… Alikuwa akijaribu kukaza macho ya Petro katika utukufu wa kidunia, ili asiweze kuuona msalaba ambao Yesu alitamani kuyaelekeza macho ya Petro. Kupitia kwa Petro, Shetani tena alikuwa akimsukumia Yesu jaribu. Lakini Mwokozi hakulisikiliza; wazo lake lilikuwa kwa mwanafunzi wake. Shetani alikuwa ameingilia kati ya Petro na Bwana wake, ili moyo wa yule mwanafunzi usiguswe na njozi ya kudhalilishwa kwa Kristo kwa ajili yake. Maneno ya Kristo hayakutamkwa kwa ajili ya Petro, bali kwa ajili ya yule aliyekuwa akijaribu kumtenganisha na Mkombozi wake. “Nenda nyuma yangu, Shetani.” Usiendelee kuingilia kati yangu na mtumishi wangu anayekosea. Hebu nimjie Petro ana kwa ana ili nimfunulie siri ya upendo wangu.

Kwa Petro, hili lilikuwa fundisho chungu na ambalo alijifunza taratibu, kwamba njia ya Kristo hapa duniani inapita kwenye mateso na fedheha. Mwanafunzi huyu alinywea kutoka katika ushirika na Bwana katika mateso. Lakini katika joto la tanuru la moto, alikuwa ajifunze baraka yake. Muda mrefu baadaye, wakati mwili wake ulipokuwa umeinama kutokana na mzigo wa umri na kazi, aliandika, “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.” (1 Petro 4:12, 13).

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.