YUDA, MWANAFUNZI MWENYE UBINAFSI


Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti.
Yohana 6:64.

Wakati Yesu alipokuwa akiwaandaa wanafunzi kwa ajili ya kuwatawaza, mmoja ambaye hakuwa ameitwa alishurutisha juu ya kuwepo kwake kati yao. Huyu alikuwa Yuda Iskariote, mtu aliyedai kuwa mfuasi wa Kristo… Yuda aliamini kuwa Yesu alikuwa ni Masihi; na kwa kujiunga na mitume, alitarajia kupata cheo cha juu katika ufalme mpya…

Wanafunzi walikuwa na shauku kwamba Yuda awe mmoja wao katika idadi yao. Alikuwa mtu mwenye mwonekano wenye mvuto mkubwa, mtu mwenye utambuzi makini na uwezo wa utendaji na wakampendekeza kwa Yesu kama mtu ambaye angemsaidia kwa kiasi kikubwa kwenye kazi yake… Historia ya baadaye ya Yuda ilikuja kuwaonesha hatari ya kuruhusu fikra za kidunia kuchukua uzito katika kuamua kufaa kwa watu kwa ajili ya kazi ya Mungu…

Hata hivyo, wakati Yuda alipojiunga na wanafunzi, hakuwa katika hali ya kutojua uzuri wa tabia ya Kristo. Aliuhisi mvuto wa ile nguvu ya Mungu ambayo ilikuwa ikivuta roho kwa Mwokozi… Mwokozi aliusoma moyo wa Yuda; Alijua kina cha uovu ambao kwa huo kama asingekombolewa kwa neema ya Mungu, Yuda angezama. Katika kumuunganisha mtu huyu naye mwenyewe, alimuweka mahali ambapo angeweza siku kwa siku, kuletwa katika muunganiko na bubujiko la upendo wake mwenyewe usio na ubinafsi.

Kama angefungua moyo kwa Kristo, neema ya Mungu ingefukuzia mbali pepo la ubinafsi na hata Yuda angeweza kuwa raia wa ufalme wa Mungu. Mungu anachukua watu kama walivyo… na kuwafundisha kwa ajili ya utumishi wake, kama watanidhamishwa na kujifunza kwake. Huwa hawachaguliwi kwa sababu ni wakamilifu, lakini bila kujali upungufu, kupitia kwa ujuzi na kuitenda ile kweli, kupitia kwa neema ya Kristo, waweze kubadilishwa na kuwa na sura yake.

Yuda alikuwa na fursa zile zile kama walizokuwa nazo wanafunzi wengine. Alisikia masomo yale yale yenye thamani. Lakini utekelezaji wa ile kweli, jambo ambalo Kristo alilitaka, ulitofautiana na tamaa na makusudi ya Yuda, naye hakukubali kusalimisha dhana zake ili kupokea hekima kutoka Mbinguni.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: ocean, cloud, sky, text, water, outdoor and nature
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.