NDANI YA PATAKATIFU PA PATAKATIFU.



Fundisho la patakatifu lilikuwa ufunguo uliofungua siri ya kukatishwa tamaa ya mwaka 1844. Lilifungua kuona mtiririo kamili wa ukweli, ulioungana na kukubaliana ukionyesha kwamba mkono wa Mungu ulikuwa umeongoza vuguvugu kuu la marejeo na ukifunua wajibu wa sasa kama ulivyofunua msimamo wa kazi ya watu wake. Kama wanafunzi wa Yesu baada ya usiku wa kutisha wa uchungu wao na kukatishwa tamaa "walivyofurahi walipomwona Bwana," ndivyo pia sasa walivyofurahi wale waliotazamia kwa imani kuja kwake mara ya pili. Walikuwa wamemtarajia aonekane katika utukufu ili kuwapatia thawabu watumishi wake. Wakati matumaini yao yalipokatishwa tamaa, hawakuweza kumwona Yesu, na kama Mariamu kaburini walilia. "Wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui waliko mweka." Sasa wamemwona tena ndani ya patakatifu pa patakatifu, kuhani mkuu wao mwenye huruma, aliye karibu kutokea kama Mfalme na Mkombozi. Nuru kutoka patakatifu ilimulika yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Walitambua kwamba Mungu alikuwa amewaongoza kwa sheria yake isiyokosea. Ingawa wao wenyewe hawakuelewa ujumbe walioutangaza kama walivyokuwa wanafunzi wa kwanza, lakini ulikuwa sahihi kabisa kwa kila namna. Kwa kuutangaza walitimiza makusudi ya Mungu, na kazi yao haikuwa bure mbele za Bwana. Ulisababisha "tena tumaini lililo hai," "walishangilia" kwa furaha isiyo elezeka na kujaa utukufu"

Unabii wa Danieli 8:14, "Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa," na ujumbe wa malaika wa kwanza, "mcheni Mungu na kumtukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja," ulihusu huduma ya Kristo ndani ya patakatifu pa patakatifu, kwenye hukumu ya upelelezi, na wala sio kwa ajili ya kuja kwa Kristo kwa ajili ya Ukombozi wa watu wake na maangamizo ya waovu.
Makosa hayakutokana na kuhesabu vipindi vya Unabii, bali yalikuwa kwenye tukio ambalo lingetokea mwishoni mwaka siku 2300. Kutokana na kosa hili waumini walipata uchungu wa kukatishwa tamaa, lakini yote yaliyo tabiriwa na Unabii, na yote waliyo yatarajia yakiridhiwa na andiko lo lote, yalikuwa yametimizwa, katika muda ule ule walipokuwa wakiomboleza kushindwa kwa matumaini yao, tukio lililokuwa limetabiriwa na ujumbe na ambalo ni lazima litimie kabla ya Bwana kutokea kuwapatia thawabu watumishi wake lilitokea.

Kristo alikuwa amekuja, sio duniani, kama walivyotegemea, bali, kama ilivyoonyeshwa katika ishara ya kielelezo, alikuja katika patakatifu pa patakatifu pa hekalu la Mungu mbinguni. Anawakilishwa na nabii Danieli kama anayekuja katika Wakati huu kwa Mzee wa Siku: "Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwana wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbinguni, na akaja" Danieli 7:13 (KJV).

Kuja huku kulitabiriwa pia na nabii Malaki: "Naye Bwana mnayemtafuta ataliijia hekalu lake ghafla; naam, yule mjumbe wa agano Mnaye mfurahia; tazama, atakuja, asema Bwana wa Majeshi." Malaki 3:1 (KJV) kuja kwa Bwana katika hekalu lake kulikuwa kwa ghafla, bila kutazamiwa kwa watu wake. Walikuwa hawamngojei pale. Walimtazamia kuja duniani, "katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasiotii injili ya Bwana wetu Yesu." "2 Wathesalonike 1:8.

Lakini watu walikuwa bado hawako tayari kumlaki Bwana wao. Bado kulikuwa na kazi ya matayarisho waliyopaswa kuikamilisha kwa upande wao. Nuru ingetolewa, ikiongoza akili zao kwenye hekalu la Mungu mbinguni, na kwa kadri ambavyo wangemfuata kwa imani kuhani wao mkuu katika huduma yake pale majukumu mapya yangefunuliwa. Ujumbe mwingine wa onyo na maelekezo ungetolewa kwa kanisa.

Itaendelea tafadhari baki nasi.......

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text and water
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.