WATOZA USHURU HAWAKUTENGWA



Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
Hosea 6:6.

Kuitwa kwa Mathayo kama mmoja wa wanafunzi wa Kristo kuliibua hasira kubwa. Kiongozi wa kidini kuchagua mtoza ushuru kama mmoja wa watumishi wake wa karibu lilikuwa ni chukizo dhidi ya desturi za kidini, kijamii na kitaifa.

Katika unyenyekevu wake ulioambatana na shukrani, Mathayo alitamani kuonesha shukrani yake kwa heshima aliyopewa; naye, huku akiita pamoja wale waliokuwa wenzake katika shughuli, katika starehe, na katika dhambi, aliandaa karamu kubwa kwa ajili ya Mwokozi. Kama Yesu aliweza kumuita yeye, aliyekuwa mwenye dhambi hivyo na asiyestahili, ni hakika angewakubali rafiki zake wa zamani, ambao, kama Mathayo alivyoona, walistahili sana zaidi yake mwenyewe. Mathayo alikuwa na shauku kubwa ya kushiriki manufaa ya rehema na neema ya Kristo. Hamu yake ilikuwa wao wajue kwamba Kristo hakudharau na kuwachukia watoza ushuru na wenye dhambi. Aliwataka wamjue Kristo kama Mwokozi mbarikiwa….

Kamwe Yesu hakukataa mwaliko kwa ajili ya karamu ya namna hiyo. Lengo alilokuwa nalo daima mbele zake lilikuwa ni kupanda mbegu za ile kweli mioyoni mwa wasikilizaji wake – kwa njia ya mazungumzo yanayoongoa ili ajitwalie mioyo yao. Katika kila tendo, Kristo alikuwa na kusudi na fundisho alilolitoa kwenye tukio hili lilifika kwa wakati mwafaka na lilikuwa sahihi. Kwa kitendo hiki alitoa tamko kwamba hata watoza ushuru na wenye dhambi hawakutengwa toka katika uwepo wake…

Mafarisayo walimwona Kristo akiketi na kula na watoza ushuru na wenye dhambi… Hawa watu waliojihesabia haki nafsini mwao, ambao hawakujisikia kuwa na hitaji la msaada, hawakuthamini kazi ya Kristo. Walijiweka wenyewe mahali ambapo wasingeukubali wokovu ambao alikuja kuuleta. Hawakuweza kumjia ili wapate uzima. Maskini! Hawa watoza ushuru na wenye dhambi walijisikia hitaji lao la kupata msaada na wakakubali maelekezo na msaada ambao walijua kuwa Kristo alikuwa na uwezo wa kuwapatia.

Mfano wa Yesu kwenye karamu ulikuwa fundisho la kudumu kwa Mathayo mwenyewe. Huyu mtoza ushuru aliyedharauliwa akawa mmoja kati ya wainjilisti waliojitoa sana, katika huduma yake mwenyewe akifuata kwa karibu hatua za Bwana wake.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.