“NIFUATE”



Baada ya hayo akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaacha vyote, akaondoka, akamfuata.
Luka 5:27, 28.

Kwa maafisa wa Kirumi katika Palestina, hakuna waliokuwa wakichukiwa kuliko watoza ushuru. Ukweli kwamba kodi zilishinikizwa na mamlaka ya kigeni lilikuwa jambo lilliloudhi bila kukoma kwa Wayahudi, likiwa jambo lililowakumbusha kuwa uhuru wao ulikuwa umeondoka. Nao waliokusanya kodi walikuwa… walikuwa na sifa yao wenyewe ya kuwa watoza kodi kwa nguvu, wakijitajirisha wenyewe kwa migongo ya watu wale. Myahudi aliyeikubali kazi hii kutoka kwa Warumi alifikiriwa kuwa msaliti wa heshima ya taifa lake. Alidharauliwa kama mwasi na aliwekwa kwenye kundi moja na watu wabaya kabisa katika jamii.

Katika kundi hili walikuwepo Lawi – Mathayo, ambaye, baada ya wanafunzi wanne kule Genesareti, ndiye aliyefuatia kuitwa kwenye huduma ya Kristo. Mafarisayo walikuwa wamemhukumu Mathayo kutokana na ajira yake, lakini Yesu aliona ndani ya mtu huyu, moyo uliokuwa tayari kupokea kweli. Mathayo alikuwa amesikiliza mafundisho ya Mwokozi. Kadiri Roho wa Mungu alivyodhihirisha uovu wake, alitamani kupata msaada kutoka kwa Kristo; lakini alikuwa amezoea ile hali ya kujitenga kwa walimu wa Kiyahudi, na hakuwa na wazo kwamba huyu Mwalimu Mkuu angemtambua.

Siku moja, akiwa ameketi kwenye kibanda cha kulipia ushuru, huyu mtoza ushuru alimwona Yesu akija. Alishangazwa sana kusikia maneno haya yakimwelekea yeye, “Nifuate.” Mathayo “akaacha vyote, akaondoka, akamfuata.” Hapakuwa na kusita, hapakuwa na maswali, hapakuwa na biashara yenye kuleta faida kubwa ili mtu aikimbilie badala ya umaskini na maisha magumu. Ilitosha kwake kwamba alikuwa awe pamoja na Yesu, ili apate kusikiliza maneno yake na kuungana naye katika kazi yake….

Kwa Mathayo katika utajiri wake, na kwa Andrea na Petro katika umaskini wao, jaribio lile lile lililetwa; kujitoa kwa namna ile ile kulifanywa na kila mmoja wao. Wakati wa mafanikio, wakati nyavu zilipojazwa kwa samaki na misukumo ya maisha ya wakati uliopita ikiwa katika kilele cha nguvu zake, Yesu aliwaomba wanafunzi pale baharini waache yote kwa ajili ya kazi ya injili. Kwa hiyo, kila roho inajaribiwa kama kutamani mambo mazuri ya muda mfupi au ushirika pamoja na Kristo ione ni lipi lenye nguvu zaidi.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: 1 person, smiling, outdoor, nature and water
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.