Kama mwakilishi wetu, Kristo anasimama mahali palipo juu kuliko pote.
Alipokuja duniani kama mjumbe wa Mungu, alishikilia wokovu wa Mungu mkononi mwake.
Binadamu wote waliwekwa mikononi mwake, kwani ktk yeye kulikuwa na ukamilifu wa Uungu.... Kristo alimdhihirisha Baba kikamilifu kiasi kwamba wajumbe waliotumwa na Mafarisayo ili wamchukue walivutiwa na kuwepo kwake....
Waliposhuhudia nuru hafifu ya utukufu wa Mungu iliyokuwa imefunika utu wake, waliposikia maneno mazuri kutoka kwenye hotuba yake, walimpenda. Na...walipoulizwa na Mafarisayo, "Mbona hamkumleta?" walijibu, "Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena" (Yohana 7:45,46)

EmoticonEmoticon