NYAKATI ZA TAABU ZINAZOKARIBIA KUJA



Wakati wa taabu, ambayo itaongezeka hadi mwisho, umekaribia sana. Hatuna wakati wa kupoteza. Ulimwengu unatikiswa na roho ya vita. Unabii wa sura ya kumi na moja ya kitabu cha Daniel karibu umefikia utimilizo wake wa mwisho.-RH Nov. 24, 1904.

Wakati wa taabu, taabu ambayo mfano wake haukuwako tangu lilipoanza kuwapo taifa(Daniel 12:2) - sasa hivi uko juu yetu, nasi tu kama wale wanawali waliolala. Hatuna budi kuamka na kumuomba Bwana Yesu aweke mikono ya milele chini yetu, na kutubeba na kutupitisha ktk wakati wa maonjo ulio mbele yetu. - 3MR 306 (1906).

Ulimwengu unaendelea kuzama zaidi na zaidi kwenye uhalifu.
Siku si nyingi taabu kuu itainuka miongoni mwa mataifa - taabu ambayo haitakoma mpaka Yesu ajapo. - RH Feb 11, 1904.

Tuko ukingoni kabisa mwa wakati wa taabu na fadhaa ambazo kamwe hazikuwahi kuwa kwenye ndoto ziko mbele yetu. - 9T 43 (1909).

Tunasimama kwenye kizingiti cha zahama ya vizazi vyote. Kwa mfululizo wa haraka haraka hukumu za Mungu zitafuatana moja baada ya nyingine - moto, na mafuliko na tetemeko la ardhi, pamoja na vita na umwagaji damu. - PK 278 (c. 1914).

Kuna nyakati za tufani mbele yetu, lakini hebu tusitamke hata neno moja la kutokuwa na imani au kukatisha tamaa. - ChS 136 (1905).

Image may contain: one or more people and text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.