BADO KITAMBO KIDOGO

Ulimwengu wote wa waovu utasimama ukishitakiwa kwa makosa ya uhaini wa hali ya juu dhidi ya serikali ya mbinguni. Hawatakuwa na yeyote kumsihi awasaidie; hawatakuwa na udhuru; na hukumu ya kifo cha milele itatolewa dhidi yao.

Waovu wataona kile walichopoteza kwa sababu ya uasi wao. "yote haya" roho zilizopotea zitalia, "ningekuwa nayo. Ah nimepumbazwa ajabu! Nimebadisha amani, furaha, na heshima kwa kuchukua huzuni, aibu na kukata tamaa." Wote wataona kuwa kutengwa kwao na mbingu ni haki.
Kwa maisha yao walitamka, "Mtu huyu Yesu hatatutawala."
Image may contain: 1 person, smiling, text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.