NDANI YA PATAKATIFU PA PATAKATIFU.



Sehemu ya.......... 2 

Nabii anasema: "Lakini ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha, nao watamtolea Bwana dhahabu katika haki. " Malaki 3:2-3. Wale wanaoishi duniani wakati uombezi wa Kristo utakapokoma katika patakatifu pa mbinguni watasimama mbele za Mungu Mtakatifu bila mpatanishi. Mavazi yao ni lazima yawe meupe, tabia zao ni lazima ziwe zimetakaswa, kutoka dhambini kwa damu ya kunyunyiza. Kupitia neema ya Mungu na juhudi zao makini ni lazima wawe washindi katika vita na mwovu. Wakati hukumu ya upelelezi ikiendelea mbinguni, wakati dhambi za waumini wanaotubu zikiondolewa kutoka patakatifu, kunapaswa kuwepo kazi maalum ya utakaso, wa kuachana na dhambi kwa watu wa Mungu duniani. Kazi hii imeelezwa vizuri ktk jumbe za Ufufuo 14.

Wakati kazi hii itakapokuwa imekamilishwa, wafuasi wa Kristo watakuwa wako tayari kwa ajili ya ujio wake, Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama siku za kale, na kama katika miaka ya zamani." Malaki 3:4 Ndipo kanisa ambalo Bwana wetu anakuja kujinyakulia litakuwa "Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi, wala lo lote kama hayo." Waefeso 5:27 Ndipo litaonekana kama "asubuhi" mzuri kama mwezi safi, kama jua la kutisha, kama jeshi lenye bendera." Wimbo Ulio bora 6:10.

Licha ya kuja kwa Bwana kwenye hekalu lake, Malaki anatabiri pia kuja kwake mara ya pili, kuja kwake kwa ajili ya kutekeleza hukumu kwa maneno haya: "Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi Mimi asema Bwana wa Majeshi." Malaki 4:5. Yuda anarejea tukio hilo pale asemapo, "Angalia, Bwana anakuwa na maelfu Kumi ya watakatifu wake, kutekeleza hukumu juu ya watu wote, na kuwaadibisha wote wasiomcha Mungu kati yao kwa ajili ya matendo yao yote ya upotovu." Yuda 14:15. Kuja huku, na kuja kwa Bwana kwenye hekalu lake, vinatofautiana na ni matukio tofauti.

Kuja kwa Kristo kama kuhani watu mkuu katika patakatifu mno, kwa ajili ya kupatakasa patakatifu, kumeelezwa katika Daniel 7:13; na kule kuja kwa Bwana katika hekalu lake, kuliko tabiriwa na Malaki, yote ni maelezo ya tukio moja; na hili pia linawakilishwa na kuja kwa Bwana arusi harusini, kulikoelezwa na Kristo katika mfano kumi na wawili wa Mathayo 25.

Itaendelea tafadhari baki nasi......

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: 1 person, text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.