PATAKATIFU NI NINI?!



Sehemu ya................. 10 

Huduma ya kuhani kwa mwaka mzima katika chumba cha kwanza cha patakatifu, "ndani ya pazia" ambayo ilikuwa na mlango wa kutenganisha patakatifu na ua wa nje, iliwakilisha kazi ya huduma ambayo Kristo aliifanya alipoingia mbinguni wakati wa kupaa kwake. Kuhani katika huduma yake ya kila siku, alileta damu ya sadaka ya dhambi mbele za Mungu, pamoja na uvumba uliopaa juu pamoja na maombi ya Israeli.
Ndivyo hivyo pia Kristo aliombea damu yake mbele ya Baba, kwa ajili ya wenye dhambi, na kuweka pamoja na harufu nzuri ya haki Yake mwenyewe pia, na maombi ya waumini wanaotubu. Hiyo ndiyo ilikuwa huduma iliyofanyika katika chumba cha kwanza cha patakatifu mbinguni.

Huko imani ya wanafunzi wa Kristo ilimfuata alipopaa kutoka machoni pao. Hapa ndipo matumaini yao yalipojengeka. Paulo anasema, "Matumaini tuliyo nayo, kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia; alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani Mkuu hata milele." "Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika patakatifu, akiisha kupata Ukombozi wa milele kwa ajili yetu." Waebrania 6:19-20; 9:12(KJV).

Kazi ya huduma hii iliendelea kwa muda wa karne kumi na nane katika chumba cha kwanza cha patakatifu. Damu ya Kristo ikisihi kwa ajili ya waumini wanaotubu, ilipata msamaha wao na kukubaliwa na Baba, lakini hata hivyo dhambi zao zilibakia katika vitabu vya kumbukumbu. Na kama ilivyokuwa katika huduma ya mifano, (ya patakatifu pa duniani) kulikuwa na kazi ya upatanisho katika mwisho wa mwaka, hivyo kabla ya kazi ya Kristo kwa ajili ya Ukombozi wa mwanadamu kukamilika kuna kazi ya upatanisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi katika patakatifu, hii ndiyo huduma iliyoanza wakati siku 2300 zilipoisha. Wakati huo, kama ilivyotabiriwa na Danieli nabii, Kuhani wetu Mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu, kufanya sehemu ya mwisho ya kazi yake kuu - kutakasa patakatifu.

Kama ilivyokuwa zamani dhambi za watu ziliwekwa kwa imani juu ya sadaka ya dhambi na kuhamishwa kupitia damu yake.
Katika mfano huo wa patakatifu pa duniani, pia katika agano jipya dhambi za watu wanaotubu kwa imani huwekwa juu ya Kristo na kuhamishwa kwenye patakatifu mbinguni halisi.
Na kama vile mfano wa utakasaji wa patakatifu pa duniani ulivyo kamilishwa kwa uondoaji wa dhambi ambazo zilikuwa zimepachafua, ndivyo pia utakasaji halisi wa mbinguni utakamilishwa kwa uondolewaji, au kufuta dhambi zilizoandikwa pale.

Lakini kabla ya kazi hii kukamilishwa, ni lazima kuwepo na uchunguzi wa vitabu vya kumbukumbu ili kutambua wale ambao kupitia toba ya dhambi na imani katika Kristo, wanapewa haki ya manufaa ya upatanisho wake. Pia utakasaji wa patakatifu unahusisha kazi ya uchunguzi - kazi ya hukumu. Kazi hii lazima itekelezwe kabla ya kuja kwa Kristo kukomboa watu wake; kwa maana ajapo, ujira wake u pamoja naye kumlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. Ufunuo 22:12. Hivyo wale waliofuata katika nuru ya neno la unabii waliona kwamba, badala ya Kristo kuja duniani mwishoni mwa siku 2300 mwaka 1844, aliingia katika patakatifu mno pa hekalu la mbinguni ili kutekeleza kazi ya mwisho ya upatanisho ya matayarisho kwa ajili ya kuja kwake.

Pia ilionekana kwamba, wakati sadaka ya dhambi inamlenga Kristo kama kafara na Kuhani mkuu humwakilisha Kristo kama Mwombezi, mbuzi wa azazeli humwakilisha Shetani.
Wakati Kuhani Mkuu, kwa utakatifu wa damu ya sadaka ya dhambi alipoondoa dhambi kutoka katika patakatifu aliziweka juu ya mbuzi wa azazeli. Wakati Kristo, kwa utakatifu wa damu yake mwenyewe, anapoondoa dhambi za watu wake kutoka katika patakatifu pa mbinguni mwishoni mwa huduma yake, ataziweka juu ya Shetani, ambaye katika utekelezaji wa hukumu, ni lazima abebe adhabu ya mwisho. Mbuzi wa azazeli alikuwa anapelekwa mbali katika nchi isiyokaliwa na watu, ili kamwe asirudi katika kusanyiko la Israeli. Ndivyo pia Shetani ataondolewa milele kutoka mbele za Mungu na watu wake naye ataangamizwa kabisa katika maangamizo ya mwisho ya dhambi na wenye dhambi.
💫💫💫💫💫💫💫💫💫💫

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
Powered by Blogger.