“NJOO UONE”



Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.
Yohana 1:45.

Filipo alimwita Nathanaeli… Kama Nathanaeli angewategemea marabi kwa uongozi, kamwe asingempata Yesu. Ilikuwa kwa kuona na kuamua yeye mwenyewe ndipo aliweza kuwa mwanafunzi. Ndivyo ilivyo kwa wengi leo, ambao ubaguzi unawazuia wasipate mema. Matokeo yangekuwa tofauti kiasi gani kama tu, wangeitikia sauti ya “njoo uone”!...

Kama Nathanieli alivyokuwa, tunahitaji kujifunza neno la Mungu sisi wenyewe na kuomba kwa ajili ya kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Yeye aliyemwona Nathanieli akiwa chini ya mtini atatuona kwenye mahali pa siri pa maombi. Malaika watokao kwenye ulimwengu wa nuru huwa karibu na wale ambao kwa unyenyekevu wanatafuta uongozi wa kimbingu.

Kwa kuitwa kwa Yohana na Andrea na Simoni, Filipo na Nathanaeli, ndio ukawa mwanzo wa kanisa la Kikristo. Yohana aliwaelekeza wawili kati ya wanafunzi wake kwa Mwokozi. Kisha Filipo akaitwa naye akaenda kumtafuta Nathanaeli. Yafaa mifano hii itufundishe umuhimu wa jitihada binafsi, za kufanya miito ya moja kwa moja kwa ndugu zetu, marafiki na majirani zetu….

Wapo wengi wanaohitaji huduma ya mioyo ya Kikristo yenye upendo. Wapo wengi ambao wameshuka katika uharibifu ambao wangeweza kuokolewa ikiwa majirani, wanaume na wanawake wa kawaida wangekuwa wameweka jitihada binafsi kwa ajili yao. Wapo wengi wanaosubiri kuelezwa peke yao. Kwenye familia zetu hizo hizo, ujirani wetu huo huo, miji yetu hiyo hiyo, tunapoishi, ipo kazi kwa ajili yetu kufanya kama wamisionari kwa ajili ya Kristo. Kama sisi ni Wakristo, kazi hii itakuwa ndiyo furaha yetu. Mara mtu anapoongoka inazaliwa ndani yake shauku ya kuwafanya wengine wajue rafiki wa thamani kubwa ambaye amempata ambaye ni Yesu. Ukweli unaookoa na unaotakasa hauwezi kufungiwa ndani ya moyo wake…

Sasa, kwamba Yesu alipaa mbinguni, wanafunzi wake ndio wawakilishi wake kati ya watu, na mojawapo ya njia zinazofaa sana katika kuongoa roho kwake ni kwa kufuata kielelezo chake katika maisha yetu ya kila siku… Maisha ya uaminifu usioyumba, yaliyojaa unyenyekevu wa Kristo, ni nguvu katika ulimwengu.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: outdoor, nature and text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.