Yohana kweli hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyoyasema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli. Nao wengi wakamwamini huko.
Yohana 10:41, 42.
Akimtangazia Zakaria kabla ya kuzaliwa kwa Yohana, malaika alitamka, “Atakuwa mkuu mbele za Bwana” (Luka 1:15). Kwa mtazamo wa Mbinguni, ni kitu gani kinachofanya ukuu? Sio kile ambacho dunia inakiita ukuu; sio mali, au cheo au kuzaliwa kwenye uzao wa kiungwana, au karama za kiakili, zikifikiriwa zenyewe… ni thamani ya maadili ambayo Mungu anathamini. Upendo na usafi ni sifa anazozithamini zaidi. Yohana alikuwa mkuu machoni pa Bwana, wakati, mbele za wajumbe kutoka Sanhedrin, mbele za watu, na mbele za wanafunzi wake wenyewe, alijiepusha na kujichukulia heshima, lakini alielekeza kwa Yesu kuwa ndiye Aliyeahidiwa. Furaha yake ambayo haikuwa na ubinafsi katika huduma ya Kristo inawasilisha aina ya uungwana ambao haujapata kudhihirishwa na mtu….
Kando ya furaha ambayo Yohana aliiona kwenye utume wake, maisha yake yalikuwa ya huzuni. Sauti yake ilikuwa imesikika mara chache isipokuwa jangwani. Maisha yake yalikuwa ya upweke. Naye hakuruhusiwa kuona matokeo ya kazi yake mwenyewe. Hakupewa fadhila ya kuwa na Kristo na kushuhudia kudhihirishwa kwa uwezo wa Mungu ukionesha nuru kuu. Hakupewa fadhila ya kuona wasioona wakirejeshewa uwezo wa kuona, wagonjwa wakiponywa na wafu wakifufuliwa. Hakuona nuru ambayo iling’aa kupitia katika kila neno la Kristo, ikieneza utukufu kwenye ahadi za unabii. Mwanafunzi mdogo kabisa aliyeona matendo makuu ya Kristo na kusikia maneno yake kwa maana hii alikuwa ni mtu aliyependelewa kuliko Yohana Mbatizaji na kwa sababu hiyo alisemwa kuwa mkuu kuliko yeye.
Yohana hakupewa uwezo huu wa kuita moto kutoka mbinguni, au kufufua wafu, kama Eliya alivyofanya, wala kuinua fimbo ya mamlaka ya Musa katika jina la Mungu. Yeye alitumwa kutangaza ujio wa Mwokozi na kuita watu wajiandae kwa ajili ya ujio wake. Yeye alikamilisha utume kwa uaminifu kiasi ambacho watu walipokumbuka kile alichowafundisha juu ya Yesu, waliweza kusema, “Yote aliyoyasema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli.” Kila mwanafunzi wa Bwana ameitwa kuchukua ushuhuda wa namna hii kwa ajili ya Kristo.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon