Sehemu ya............ 9
Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.
Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo na watu" Mambo ya Walawi 16:21-22. Mbuzi wa azazeli harudi kamwe katika kambi ya Israeli, na yule mtu aliyempeleka huko mbali alipaswa kuoga na kufua nguo zake kwa maji kabla ya kurejea kambini.
Utaratibu wote ulikusudiwa kuwakazia Waisraeli kwenye utakatifu wa Mungu, na chuki yake kwa dhambi; na pia kuwaonyesha kwamba hawawezi kushirikiana na dhambi pasipo kunajisika. Kila mtu alitakiwa kujitesa roho yake wakati kazi hii ya upatanisho ilipokuwa ikiendelea. Shughuli zote ziliachwa, na kusanyiko lote la Israeli walipaswa kuitumia siku hiyo kwa kujinyenyekeza kabisa mbele za Mungu, kwa maombi, kufunga, na kuchunguza moyo kwa kina kabisa.
Kweli muhimu zinahusu upatanisho zinafundishwa kwa njia ya huduma ya vielelezo. Kubadilishana kulikubaliwa kwa niaba ya mwenye dhambi; lakini dhambi haikufutwa kwa damu ya kafara ya Mnyama. Kwa hiyo njia ya namna ya kuhiamishia patakatifu ilitolewa. Kwa njia ya kutoa sadaka ya damu mwenye dhambi alikiri mamlaka ya sheria, akaungama kuwa amevunja sheria, na akaonyesha shauku yake ya msamaha kwa njia ya kumwamini Mkombozi atakaye kuja; lakini bado alikuwa hajafunguliwa kabisa aondokane na hukumu ya kuvunja sheria. Siku ya upatanisho kuhani mkuu, akiisha kupokea sadaka kutoka kwenye kusanyiko, aliingia patakatifu mno akiwa na damu ya sadaka hii, na kuinyunyizia juu ya kiti cha rehema, moja kwa moja juu ya sheria, ili kuitimizia madai yake.
Halafu, kwa sifa yake kama mwombezi, alizichukua dhambi juu yake na kuzibeba kutoka patakatifu. Akiwa ameweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa azazeli, huungama juu ya dhambi hizi zote, kwa njia ya kichwa cha mbuzi wa azazeli, huungama juu ya dhambi hizi zote, kwa njia hii huzinamisha kutoka kwake kwenda kwa mbuzi.
Kisha mbuzi huzichukua na kuzipeleka huko mbali, na hivyo kuhesabiwa kana kwamba zimetenganishwa na watu milele.
Hivyo ndivyo huduma ilivyofanyika "Katika mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni." Na kile kilichofanyika kwa njia ya mfano katika huduma ya patakatifu pa duniani kinafanyika katika uhalisia katika huduma ya patakatifu pa mbinguni. Baada ya kupaa kwake Mwokozi wetu alianza kazi yake kama kuhani wetu Mkuu. Paulo anasema, "Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu." Waebrania 9:24.
Itaendelea tafadhari baki nasi......
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon