Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
Mathayo 10:28.
Kwa akili za wengi, fumbo la kina sana linaonekana kuzunguka hatima ya Yohana Mbatizaji. Hawa wanahoji kwa nini ilipasa aachwe kudhoofika na kufa gerezani. Macho yetu ya kibinadamu hayawezi kupenya na kuona ndani ya fumbo hili la majaliwa ya Mungu; lakini hata hivyo, haliwezi kutingisha imani yetu katika Mungu tunapokumbuka kwamba Yohana alikuwa mshirika katika mateso ya Kristo…
Yesu hakuingilia ili kumwokoa mtumishi wake. Alijua kwamba Yohana angeshinda mtihani. Mwokozi angemjia Yohana kwa furaha, ili kung’aza giza la gereza la chini ya ardhi kwa kuwepo kwake. Lakini yeye mwenyewe asingejitia mikononi mwa maadui na kuhatarisha utume wake mwenyewe. Angefurahi kumwokoa mtumishi wake mwaminifu. Lakini kwa ajili ya maelfu ambao katika miaka ya baadaye wangepita kutoka gerezani kwenda mautini, ilimpasa Yohana anywee kikombe cha ufia dini. Wafuasi wa Yesu wanapoteseka kwenye vyumba vya magereza, au kuangamia kwa upanga, vitanda vya kutesea, au kwenye kuni za moto, … Lingekuwa jambo bora kiasi gani kuwa na wazo kwamba Yohana Mbatizaji, ambaye kwa uaminifu wake Kristo mwenyewe alimshuhudia, alipitia uzoefu kama huo huo!
Shetani aliruhusiwa kufupisha maisha ya duniani ya mjumbe wa Mungu; lakini maisha yale ambayo “yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu,” mharibu asingeweza kuyafikia. Wakolosai 3:3. Alishangilia kwamba aliweza kumletea Kristo simanzi, lakini alishindwa kumshinda Yohana. Mauti pekee iliweza tu kumweka pale ambapo palikuwa mbali na nguvu ya jaribu….
Kamwe Mungu hawapeleki watoto wake mahali pengine kuliko pale wanapochagua kupelekwa, kama wangeweza kuona mwisho tangu mwanzo na kutambua utukufu wa kusudi ambalo wanalikamilisha kama watendakazi pamoja na Yeye. Sio Henoko, ambaye alibadilishwa na kuingizwa mbinguni, wala Eliya, ambaye alipanda katika gari la moto, ambao walikuwa wakuu au waliheshimika kuliko Yohana Mbatizaji, ambaye aliangamia mwenyewe kwenye gereza chini ya ardhi. “Mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake” (Wafilipi 1:29). Lakini katika karama zote ambazo Mbingu inaweza kutoa kwa watu, ushirika pamoja na Kristo katika mateso yake ni amana yenye uzito wa juu zaidi na heshima ya juu kuliko zote.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon