PATAKATIFU NI NINI?!



Sehemu ya............. 8

Huduma za hema takatifu la duniani zilihusisha pande mbili; makuhani walihudumu kila siku ndani ya Patakatifu, na mara moja kwa mwaka kuhani mkuu alifanya kazi maalumu ya upatanisho ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, kwa ajili ya kupatakasa Patakatifu. Siku kwa siku mwenye dhambi aliyetubu alileta sadaka yake kwenye mlango wa hema, na kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kafara, aliungama dhambi zake, kwa kielelezo hicho alizihamisha kutoka kwake hadi kwenye kafara isiyo na hatia.
Kisha mnyama huyo wa kafara alichinjwa. Mtume anasema, "Bila kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi." "Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu." Mambo ya Walawi 17:11. Sheria ya Mungu iliyovunjwa ilidai uhai wa mkosaji.

Damu huwa badala ya uhai wa mwenye dhambi ambaye hatia yake imechukuliwa na yule mnyama wa sadaka, Kuhani alichukua damu hiyo mpaka Patakatifu akainyunyiza mbele ya pazia, ambalo nyuma yake kulikuwa na sanduku lililokuwa na sheria ambayo mwenye dhambi alikuwa amevunja. Kwa utaratibu huu, kwa njia ya damu, dhambi ilihamishwa kwa njia ya kielelezo na kuwekwa katika Patakatifu.
Wakati mwingine damu haikupelekwa katika Patakatifu; ila kuhani aliila nyama ya sadaka, kama Musa alivyowaelekeza wana wa Haruni, akisema: "Mungu amewapatia ninyi ili kuuchukua uovu wa mkutano." Mambo ya Walawi 10:17.
Taratibu zote mbili, (kunyunyiza damu na kula nyama) ziliwakilisha uhamishaji wa dhambi kutoka kwa mwenye dhambi na kuiweka katika Patakatifu.

Hiyo ndiyo kazi iliyoendelea siku kwa siku, mwaka mzima. Dhambi za Waisraeli zilihamishwa namna hiyo na kuwekwa katika Patakatifu, na ikalazimika kazi maalumu ifanyike kwa ajili ya kuziondoa. Mungu aliamuru kwamba upatanisho ufanyike kwa ajili ya Utakatifu wa kila chumba. "Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali Patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam kwa ajili ya dhambi zao zote: naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja na katikati ya machafu yao." Upatanisho pia ulipaswa kufanywa kwenye madhabahu, "kuitakasa na kuiweka wakfu ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke." Mambo ya Walawi 16:16,19.

Mara moja kwa mwaka, katika siku kuu ya upatanisho, kuhani mkuu aliingia Patakatifu mno ili kupatakasa Patakatifu. Kazi iliyofanyika pale ilikamilisha mzunguko wote wa huduma kwa mwaka mzima katika siku ya upatanisho wana mbuzi wawili waliletwa kwenye mlango wa hema ya kukutania, na kupigiwa kura, "Kura moja kwa Bwana, na nyingine kwa azazeli." Walawi 16:8. Mbuzi yule ambaye kura ya Bwana ilimuangukia angechinjwa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu. Na kuhani alipaswa kinyunyizwa juu ya madhabahu ya uvumba ambayo ilikuwa mbele ya pazia.

Itaendelea tafadhari baki nasi.........

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.