Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake.
Wafilipi 1:29.
Yohana Mbatizaji alikuwa wa kwanza kuutangaza ufalme wa Kristo na alikuwa wa kwanza pia kuteseka… Sasa alifungiwa kwenye kuta za gereza la chini ya ardhi…Kadiri juma moja baada ya lingine yalivyopita, huku pakiwa hapana badiliko, kukata tamaa na wasiwasi vilimteka. Wanafunzi wake, hawakumwacha… Lakini walihoji kwa nini, ikiwa huyu mwalimu mpya alikuwa ndiye Masihi, hakufanya chochote kusababisha Yohana awekwe huru….
Kama wanafunzi wa Mwokozi walivyokuwa, Yohana Mbatizaji hakuelewa asili ya ufalme wa Kristo. Alimtegemea Yesu kuwa angetwaa kiti cha enzi cha Daudi; na kadiri muda ulivyopita, na Mwokozi hakudai mamlaka ya kifalme, Yohana alifadhaika na kuwa na wasiwasi…. Zipo saa ambazo minong’ono ya mapepo ilihangaisha nafsi yake na kivuli cha hofu ya kutisha kilimjia. Je, ingewezekana kwamba Mkombozi aliyetegemewa kwa muda mrefu alikuwa bado hajaja?...
Lakini Yohana Mbatizaji hakuiacha imani yake katika Kristo… Alikusudia kumtumia Yesu ujumbe wenye swali. Aliwaamini wanafunzi wake wawili katika kuupeleka… Wanafunzi hawa walimjia Yesu wakiwa na ujumbe wao, “Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”…. Mwokozi hakujibu swali la wanafunzi mara moja. Walipokuwa wamesimama wakishangaa ukimya wake, wagonjwa na walioteswa walikuwa wakija kwake ili waponywe…Alipokuwa akiponya maradhi yao, aliwafundisha watu…
Kwa namna hiyo siku ilipita, wanafunzi wa Yohana wakiona na kusikia yote. Hatimaye Yesu aliwaita wamkaribie na kuwaomba waende na kumwambia Yohana kile walichoshuhudia…. Uthibitisho wa Uungu wake ulionekana kwa namna ulivyopatana na mahitaji ya shida za wanadamu…
Wanafunzi walichukua ujumbe, na hiyo ilitosha… Si tu kwamba kazi za Kristo zilimtangaza kuwa Masihi, bali pia zilionesha ni kwa namna gani ufalme wake ulikuwa usimikwe… Sasa akiwa ameelewa zaidi asili ya utume wa Kristo, yeye [Yohana] alijisalimishwa mwenyewe kwa Mungu iwe ni kwa uzima au kwa mauti, kwa namna ambayo ingeshughulikia maslahi ya kazi aliyoipenda.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon