Sehemu ya............... 7
Swali, Patakatifu ni nini? Linajibiwa vizuri na Maandiko. Neno "Patakatifu," kama lilivyotumika katika Biblia, kwanza humaanisha hema lililojengwa na Musa, kama kielelezo cha mambo ya mbinguni; na pili humaanisha "hema halisi" mbinguni, ambalo ndilo lilifanya kuwepo kwa hema la duniani. Wakati wa kifo cha Kristo huduma ya mifano na vielelezo ilikoma. "hema halisi" mbinguni ni hema takatifu la agano jipya.
Na kwa kadri Unabii wa Danieli 8:14 unavyotimia katika huu mpango wa Mungu, hema takatifu ambalo linazungumziwa ni lazima liwe hema takatifu la agano jipya. Kufikia mwishoni mwa siku 2300, mwaka 1844, hapakuwa na hema takatifu duniani kwa karne nyingi. Kwa hiyo Unabii "Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo Patakatifu patakapotakaswa," bila pingamizi hulenga kwenye hekalu la mbinguni.
Lakini swali la muhimu linabaki bila kujibiwa: Kutakasa hekalu ni nini?!
Kuhusiana na kuwepo kwa huduma hiyo katika hema takatifu la duniani kunaelezwa katika Maandiko ya agano la kale. Lakini, Je, kunaweza kuwepo kitu chochote cha kutakaswa mbinguni?! Katika Waebrania 9 kutakaswa kwa mahekalu yote mawili: hema takatifu la duniani na la mbinguni kunafundishwa vizuri kabisa. "Na katika torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi ikiwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo (damu ya wanyama): Lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo." Waebrania 9:22-23, yaani damu ya thamani kuu ya Kristo.
Utakasaji katika huduma zote mbili; katika huduma kielelezo na katika huduma halisi, ni lazima zikamilishwe kwa damu: katika huduma kielelezo utakasaji ulifanywa kwa damu ya wanyama; na katika huduma halisi utakasaji hufanywa kwa damu ya Kristo. Paulo anaeleza, sababu ya utakasaji huu lazima kufanywe kwa kutumia damu, kwamba bila kumwaga damu hakuna ondoleo. Ondoleo au kufutilia mbali kwa dhambi, ni kazi inayopaswa kutimizwa. Lakini ni kwa namna gani dhambi inaunganishwa na Patakatifu, ama mbinguni au duniani?! Hili linaweza kueleweka kwa kurejea kwenye huduma ya kielelezo; kwa maana makuhani walio hudumu katika ofisi ya ukuhani duniani, walihudumu kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni." Waebrania 8:5.
Itaendelea tafadhari baki nasi......
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon