Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.
Mathayo 11:11.
Ni kitu gani kilichomfanya Yohana Mbatizaji kuwa mkuu? Alifunga akili yake dhidi ya wingi wa desturi zilizowasilishwa na walimu wa taifa la Kiyahudi na akaifungua kwa hekima itokayo juu.
Yohana Mbatizaji hakufanywa kufaa kwa wito wake wa juu kama mtangulizi wa Kristo kwa kuhusiana na watu wakuu wa taifa katika shule za Yerusalemu. Alikwenda nyikani, ambapo desturi na mafundisho ya watu visingeweza kujenga akili yake na ambapo angeshikilia ushirika wake na Mungu bila kuzuiwa.
Yohana Mbatizaji alikuwa mtu aliyejazwa kwa Roho Mtakatifu tangu kuzaliwa kwake na kama kulikuwa na mtu yeyote ambaye angekaa bila kuathiriwa na mivuto inayoharibu ya kizazi chake alichoishi kwacho, kwa hakika alikuwa ni yeye.
Hata hivyo, hakujaribu jambo la hatari la kutumainia nguvu zake; alijitenga na rafiki zake na jamaa zake, ili hisia zake za asili zisiwe mtego kwake. Hakujiweka kwa namna ya kutojali kwenye njia ya jaribu wala pale ambapo anasa au hata mambo yanayofaa katika maisha yangemfanya kuendekeza raha au kuridhisha uchu, kwa namna hiyo kupunguza nguvu yake ya kimwili na kiakili….
Alijisalimisha mwenyewe kwa hali ya ufukara na upweke jangwani, ambapo angejitunzia akili ya kiroho ya uzuri wa Mungu kwa kujifunza kitabu chake kikuu cha viumbe asili… Hii ilikuwa hali iliyopangwa ili kukamilisha tabia ya kimaadili na kudumisha hofu ya Bwana daima mbele zake. Yohana, mtangulizi wa Kristo, hakuacha mlango wazi kwa mazungumzo maovu na mivuto inayoharibu ya dunia hii.
Aliogopa athari yake kwenye dhamiri yake, ingefanya dhambi isionekane kuwa mbaya sana. Badala yake alichagua nyumbani kwake pawe ni jangwani, ambapo utambuzi wake usingepotoshwa na mazingira yake. Je, hatuwezi kujifunza kitu fulani kutokana na mfano huu wa mtu ambaye Kristo alimheshimu na hata akasema: “Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji”?
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon