CHINI YA MTINI



Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.
Yohana 1:47.

Nathanaeli alimsikia Yohana alipokuwa akiwaonesha watu Mwokozi na kusema, “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29)! Nathanieli alimwangalia Yesu, lakini alikatishwa tamaa na mwonekano wa Mkombozi wa ulimwengu. Je, huyu ambaye alikuwa na alama za umaskini na maisha yenye kazi ngumu angeweza kuwa Masihi?

Yesu alikuwa mfanyakazi; alikuwa amefanya kazi ngumu na wafanyakazi wanyenyekevu na Nathanieli aliondoka. Lakini hakuweza kujenga hoja yake bayana juu ya tabia ya Yesu. Alipiga magoti chini ya mtini, akimuuliza Mungu kama kweli huyu mtu alikuwa Masihi. Wakati akiwa pale, Filipo alimjia na kusema, “Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.”

Lakini neno “Nazareti” kwa mara nyingine liliamsha hali ya mashaka, naye akasema, “Laweza neno jema kutoka Nazareti?” Alikuwa amejazwa na maoni ya kibaguzi; alisema tu, “Njoo uone.”… Isingekuwa vyema kwetu kwenda chini ya mtini kumwomba Mungu atusaidie kujua ukweli ni upi? Jicho la Mungu lisingekuwa juu yetu kama lilivyokuwa juu ya Nathanaeli? Nathanaeli alimwamini Bwana, naye akasema, “Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli.”

Wapo wengi walio katika hali hiyo hiyo kama Nathanaeli. Wana maoni ya kibaguzi na kutokuamini kwa sababu kamwe hawajawahi kukutana na ukweli huu wa pekee kwa ajili ya siku hizi za mwisho au na watu wanaoushika, nayo hali hiyo itahitaji kuwepo na kukutana mahali penye ukamilifu wa Roho wa Kristo ili kufutilia mbali hali yao ya mashaka.

Bila kujali tunakabiliana na nini, tunakutana na upinzani kiasi gani, bila kujali tunakutana na jitihada kiasi gani zinazogeuza mioyo kutoka kwenye ukweli wenye asili ya mbinguni, ni lazima tuitangaze imani yetu, ili mioyo yenye uaminifu ipate kuona na kusikia na kusadiki yenyewe. Kazi yetu ni kusema kama alivyofanya Filipo: “Njoo uone.” Hakuna fundisho lolote tunalolishika ambalo tunatamani kulificha.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: sky, ocean, text, nature and outdoor
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.