KUWA WANAFUNZI WA KRISTO



Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
Marko 1:17, 18. 

Hawa walikuwa watu wanyenyekevu na wasio na elimu, wale wavuvi wa Galilaya; lakini Kristo, nuru ya ulimwengu, alikuwa na uwezo mwingi kuwafanya wawe bora kwa ajili ya nafasi ambazo kwazo aliwachagua. Mwokozi hakudharau elimu; kwani tunapotawaliwa na upendo wa Mungu na kujitoa kwa huduma yake, kuendeleza tabia ni baraka.

Lakini alipita wenye hekima wa wakati wake, kwa sababu walikuwa na hali ya kujiamini kiasi ambacho wasingeweza kuhurumia binadamu wanaoteseka na kuwa watendakazi pamoja na mtu wa Nazareti. Katika hali ya kuwa na imani kali, walidharau kufundishwa na Kristo. Bwana Yesu anataka ushirikiano wa wale watakaokuwa mifereji ambayo haitazuiwa kwa ajili ya ushirika wa neema yake…

Yesu alichagua wavuvi ambao hawakuwa na elimu kwa sababu hawakuwa wamefundishwa katika desturi na utamaduni wenye makosa wa wakati wao. Hawa walikuwa watu wenye uwezo wa asili na walikuwa wanyenyekevu na wanaofundishika, -- Watu ambao angeweza kuwaelimisha kwa ajili ya kazi yake.


Katika maisha ya kawaida, kuna watu wengi ambao kwa uvumilivu huwa kuna wengi wanaotembea katika mzunguko wa kazi ngumu za kila siku, bila kujua kwamba wanao uwezo ambao ukiwekwa katika vitendo, utamuinua hadi kufikia katika usawa na watu wa dunia wenye heshima kubwa zaidi.

Mguso wa mkono ulio stadi unahitajika ili kuinua uwezo huo uliolala. Walikuwa watu wa namna hiyo ambao Yesu aliwaita ili wawe watendakazi wake wenza; naye akawapa faida ya kushirikiana naye mwenyewe. Kamwe wakuu wa ulimwengu hawakuwa wamewahi kuwa na mwalimu wa namna hiyo. Wanafunzi walipotoka kwenye mafunzo ya Mwokozi, hawakuwa wajinga tena na wasiostaarabika.

Walikuwa sasa kama yeye kwa mawazo na tabia na watu waliwatambua kwamba hawa walikuwa pamoja na Yesu. Yeye aliyewaita wavuvi wa Galilaya bado anaita watu kwa ajili ya utumishi wake. Naye yuko tayari kudhihirisha uwezo wake kupitia kwetu kama alivyofanya kupitia kwa wanafunzi wa kwanza.

Bila kujali kuwa sisi ni waovu na wapungufu kiasi gani, Bwana anatupatia nafasi ya kuwa na ubia pamoja naye mwenyewe, nafasi ya kuwa wanafunzi kwenye shule ya Kristo. Anatualika kuja chini ya maelekezo ya kimbingu, ili, tunapounganika na Kristo, tupate kuzitenda kazi za Mungu.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text, water and outdoor
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.