"Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako,…mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo." Kumbukumbu la Torati 15:7,8.
Muda baada ya kurudi kwa waliotoka uhamishoni Babeli, Wayahudi wenye mali walikuwa wamekwenda kinyume kabisa na maagizo haya. Maskini walipolazimika kukopa ili kumlipa mfalme kodi, wenye mali waliwakopesha, lakini waliweka riba kubwa sana. Huku wakichukua ardhi za maskini wale kwa kuziweka rehani, taratibu, matajiri hawa waliwashusha hawa wadeni hadi kwenye umaskini wa kutisha. Wengi walilazimika kuuza wana na mabinti zao na kuacha waingie utumwani; na halikuonekana kuwepo tumaini lolote la kuboresha hali yao, hapakuwa na njia yoyote ya kukomboa watoto wao wala ardhi zao, hawakuwa na matumaini yoyote bali kudumu kuongezeka kwa dhiki, kudumu kuwa wahitaji na watumwa. Licha ya hayo, wote walikuwa wa taifa moja, watoto wa agano lile lile, kama walivyokuwa wale ndugu zao waliobarikiwa zaidi…
Nehemia aliposikia juu ya ukandamizaji huu wa kikatili, hasira ilijaa moyoni mwake… Aliona kwamba ili afanikiwe kuvunja hizi desturi kandamizi za utozaji wa nguvu, ilikuwa ni lazima asimamie haki. Kwa nguvu kubwa na kudhamiria, alifanya kazi ya kuleta nafuu kwa ndugu zake.
Ukweli kwamba hawa wakandamizaji walikuwa watu wenye mali, ambao walihitajika sana kuunga mkono kazi ya kurejesha mji, haukumgusa Nehemia hata kidogo. Aliwakemea kwa uwazi kabisa wale waungwana na watawala, na alipokuwa amekusanya kusanyiko kubwa la watu aliwapatia masharti ya Mungu yanayohusiana na suala hili….
Taarifa hii inafundisha jambo la muhimu. “Shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha” (1 Timotheo 6:10). Katika kizazi hiki, shauku ya kupata zaidi ni hamasa inayozidi kuteka wengi… Sisi sote tulikuwa wadeni kwa haki ya Mungu, lakini hatukuwa na chochote cha kulipia deni. Kisha, Mwana wa Mungu aliyetuhurumia, akalipa bei ya ukombozi wetu. Akawa maskini ili kupitia kwa umaskini wake tupate kuwa matajiri. Kwa vitendo vya ukarimu kwa maskini wake tupate kuthibitisha ukweli wa shukrani zetu kwa ajili ya rehema aliyotupatia.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon