“SIWEZI KUSHUKA” “SIWEZI KUSHUKA”



Na mimi nikatuma wajumbe kwao, nikasema, Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi, hata nisiweze kushuka; mbona kazi ikome, hapo ninapoiacha, niwashukie? Nehemia 6:3.

Nehemia alichaguliwa na Mungu kwa sababu alikuwa tayari kushirikiana na Bwana kama mrejeshaji… Alipoona kanuni zisizo sahihi zikitekelezwa, hakusimama pembeni kama mtazamaji na kukubaliana kwa kuwa kimya. Hakuacha watu wahitimishe kwamba alikuwa amesimama upande usio sahihi. Alichukua msimamo thabiti usioyumba kwa ajili ya kile kilicho sahihi.

Kila mbinu atakayoipendekeza mfalme wa giza, inaweza kutumika kushawishi watumishi wa Mungu kutengeneza mwungano wenye mawakala wa Shetani… Kama Nehemia alivyokuwa, inapasa wajibu kwa uthabiti, “Hii ni kazi kubwa ninayoifanya mimi, hata nisiweze kushuka.” Wafanyakazi wa Mungu wanaweza kuendelea na kazi yao kwa usalama, wakiruhusu jitihada yao ikanushe uwongo ambao kijicho kinaweza kuunda ili kuwaumiza. Kama walivyokuwa wajenzi wa kuta za Yerusalemu ni lazima wakatae kupotoshwa kutoka katika kazi yao na vitisho na dhihaka…

Mwisho unavyozidi kukaribia, majaribu ya Shetani yataletwa kwa nguvu kubwa zaidi kwa watendakazi wa Mungu. Atatumia mawakala wa kibinadamu kudhihaki na kutukana wale “wanaojenga ukuta.” Lakini je, ni sawa kwamba wajenzi washuke ili kukabiliana na mashambulizi ya maadui zao, hili litachelewesha kazi. Inawapasa wajitahidi kushinda makusudi ya maadui zao, lakini haipasi waruhusu chochote kiwaite kutoka kwenye kazi yao. Ukweli una nguvu kuliko uwongo na haki itashinda dhidi ya ubaya… Katika kujitoa kuliko kamili kwa ajili ya kazi ya Mungu na hali ya kumtegemea Mungu kikamilifu, ndipo ilipo sababu ya kushindwa kwa maadui zake kumvuta kwa nguvu yao. Nafsi yenye uzembe huwa inakuwa rahisi kuanguka kwenye jaribu; lakini maishani mwake mwenye lengo la kiungwana, kusudi linaloshughulisha, uovu haupati nafasi ya kutosha ya kuweka mguu…

Mungu ametoa usaidizi wa kimbingu kwa ajili ya dharura zote kwa namna inayozidi kabisa uwezo wa kibinadamu. Yeye huwa anamtoa Roho Mtakatifu ili asaidie katika kila njia, kuimarisha tumaini letu na uhakika wetu, ili kuangaza akili zetu na kusafisha mioyo yetu. Yeye huwa anatoa fursa na kuweka milango wazi kwa ajili ya kazi. Watu wake wakiweza kuona dalili za majaliwa yake, wakiwa tayari kushirikiana naye, watapata matokeo makubwa.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text, outdoor and nature
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.