JENGA —KARABATI– REJESHA



Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
Isaya 58:12.

Katika kazi ya matengenezo ambayo ni lazima iendelezwe leo, lipo hitaji la watu ambao kama Ezra na Nehemia, hawatarahisisha kosa au kutetea dhambi, wala kujitenga kutoka katika kuthibitisha heshima ya Mungu. Wale ambao mzigo wa kazi hii upo mabegani hawatanyamaza wanapoona ubaya ukitendwa, wala hawatafunika uovu kwa koti la hisani za uwongo. Hawa watakumbuka kwamba Mungu hana upendeleo na kwamba ukali kwa wachache unaweza kuthibitishia rehema kwa wengi. Watakumbuka pia kwamba ndani ya yule anayekemea uovu roho wa Kristo ni lazima idhihirishwe.

Katika kazi yao, Ezra na Nehemia walijinyenyekeza mbele za Mungu, wakitubu dhambi zao na dhambi za watu wao na wakiomba msamaha kana kwamba wao wenyewe ndio waliokuwa wakosaji… Nehemia hakuwa kuhani; hakuwa nabii; hakujidai kuwa na cheo kikubwa. Yeye alikuwa mwanamatengenezo aliyekuzwa kwa ajili ya wakati wa muhimu. Kuwaweka watu katika kuwa vizuri na Mungu ndilo lililokuwa lengo lake. Akiwa amevuviwa kwa kusudi lililo kuu, aliweka nguvu zake zote kwa ajili ya ukamilishwaji wa kusudi hilo… Alipokutana na uovu na upinzani dhidi ya kilicho sahihi alisimama kwa kudhamiria kiasi ambacho watu waliamshwa kufanya kazi wakiwa na ari mpya na ujasiri….

Kazi ya urejeshwaji na matengenezo ambayo ilifanywa na wale waliorudi kutoka uhamishoni, chini ya uongozi wa Zerubabeli, Ezra na Nehemia, inawasilisha taswira ya kazi ya urejeshwaji wa kiroho ambayo itafanywa siku za mwisho za historia ya dunia hii… Watu wa Mungu waliosalia, wanaposimama mbele za ulimwengu kama wanamatengenezo, yapasa waoneshe kwamba sheria ya Mungu ni msingi wa matengenezo yote ya kudumu na kwamba Sabato ya amri ya nne inapasa isimame kama kumbukumbu ya uumbaji, kumbusho la kudumu la nguvu ya Mungu. Inawapasa wawasilishe umuhimu wa utii kwa kanuni za Amri Kumi kwa kauli zilizo bayana na wazi. Huku wakibidishwa na upendo wa Kristo, inapasa washirikiane pamoja naye katika kutengeneza mahali palipobomoka; na wenye kurejeza njia za kukalia.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text, outdoor and nature
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.