Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.
Luka 1:15.
Kwenye rekodi ya mbinguni ya walio wakuu, Mwokozi alisema kwamba hakuna aliyesimama aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Kazi aliyokabidhiwa ilikuwa ile ambayo haikuhitaji tu nguvu za kimwili na ustahimilivu, bali pia viwango vya juu vya akili na roho. Maandalizi ya kumkuza sahihi kimwili yalikuwa muhimu sana kiasi kwamba alitumwa malaika mwenye cheo cha juu zaidi mbinguni akiwa na ujumbe wenye maelekezo kwa wazazi wa mtoto.
Jangwani, Yohana alikuwa tayari kujikana mwenyewe na kudhibiti hamu yake ya chakula na kuvaa kwa namna ya usahili wa asili. Vilevile hapakuwa na chochote jangwani pale ambacho kingeondoa mawazo yake kutoka kwenye kutafakari na kuomba. Shetani aliweza kumfikia Yohana, hata baada yake kufunga kila njia iliyokuwa katika uwezo wake, ambayo Shetani angeingia. Lakini mazoea maishani mwake yalikuwa masafi sana na ya kawaida yenye utulivu, kiasi kwamba aliweza kumtambua adui yule, na alikuwa na nguvu ya roho na uamuzi kitabia wa kumpinga.
Kitabu cha asili kilikuwa wazi mbele za Yohana kikiwa kimesheheni ghala isiyoisha yenye maelekezo anuai. Yeye alitafuta kibali cha Mungu na Roho Mtakatifu akawa juu yake na kuwasha moyoni mwake ari iliyong’aa ya kufanya kazi kuu ya kuita watu wapate kutubu na kuishi maisha bora na matakatifu zaidi. Yohana alijiweka sawa yeye mwenyewe, kwa hali ya kutokuwa na kitu na ugumu wa maisha yake ya upweke, ili adhibiti nguvu zake zote za kimwili na za kiakili ili apate kusimama kati ya watu akiwa hayumbishwi na mazingira kama miamba na milima ya jangwani iliyokuwa ikimzunguka kwa miaka thelathini.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon