PATAKATIFU NI NINI?!



Andiko ambalo zaidi ya mengine yote lilikuwa msingi na nguzo ya imani ya marejeo lilikuwa ni tangazo kwamba; "Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa. " Daniel 8:14. Haya yalikuwa maneno yaliyozoeleka kwa waumini wote waliongojea marejeo ya Bwana yaliyo karibu sana. 

Unabii huu uliundwa na vinywa maelfu kama neno la siri la kulinda imani yao. Wote waliona kwamba kuhusu matukio yaliyotabiriwa ndani yake ndimo kumejengwa matarajio makuu na matumaini yao waliyoshikilia kwa upendo mkuu. Siku hizi za unabii zilikuwa zimeonyeshwa kuishia ktk majira ya kipupwe ya mwaka 1844. Kwa ujumla Wanamarejeo pamoja na ulimwengu wote wa Kikristo ulichukulia kwamba dunia, au sehemu fulani ya dunia, ndio ilikuwa patakatifu. Walifahamu kuwa utakasaji wa patakatifu ulikuwa utakaso wa dunia kwa moto wa siku za mwisho, na kwamba utakaso huu ungefanyika wakati wa kuja mara ya pili. Kwa hiyo wakafikia hitimisho kwamba Kristo angerudi duniani mwaka 1844.

Lakini muda uliopangwa ulipita, na Bwana hakutokea. Waumini walijua kwamba neno la Mungu haliwezi kushindwa; tafsiri yao ya unabii ni lazima iwe imekosewa; lakini kosa lilikuwa wapi? Wengi wao kwa pupa walikata ugumu wa fundo kwa kukataa siku 2300 kuishia mwaka 1844. Hakuna sababu ambayo ingeweza kutolewa kwa kutokuja huku kwa Kristo katika muda uliotarajiwa. Wakitoa hoja kwamba kama siku za unabii zilikuwa zimeisha mwaka 1844, Kristo angekuwa amerudi kupasafisha patakatifu kwa utakaso wa dunia kwa moto; na kwa vile hakuja; basi siku zilikuwa hazijatimia.

Kukubali hitimisho hili kulikuwa ni kukataa uzingatiaji wa awali wa vipindi vya unabii. Siku 2300 zilikuwa zimeonekana kuanzia wakati amri ya Artashasta kwa ajili ya kurejea na kuujenga Yerusalemu ilipotekezwa, katika majira ya kipupwe ya mwaka 457 KK. Huu ukichukuliwa kama mwaka wa kuanzia, kuna ulinganifu kamili katika utendaji wa matukio yote yaliyotabiriwa katika ufafanuzi wa kipindi hicho katika Daniel 9:25-27.
Majuma sitini na tisa, miaka 483 ya mwanzo ya miaka 2300, ilikuwa ifikie kwa masihi, mtiwa mafuta; na Kristo alibatizwa na kutiwa mafuta na Roho Mtakatifu, mwaka 27 BK, ilikamilisha kabisa sehemu hii ya unabii. Katikati ya juma la sabini, masihi atakatiliwa mbali.
Miaka matatu na nusu baada ya ubatizo wake, Kristo alisulubiwa, katika majira ya vuli ya mwaka 31 BK. Majuma sabini, au miaka 490, itafungamana hasa na Wayahudi. Mwishoni, mwa kipindi hiki taifa lilitia muhuri kwa kumkataa kwake Kristo kwa kuwatesa wanafunzi wake, na mitume wakawageukia watu wa mataifa, mwaka 34 BK. Hivyo miaka 490 ya mwanzo ya miaka 2300 ikiwa imekwisha, ikawa imesalia miaka 1810. Malaika alisema, Ndipo patakatifu patakatifu. "Sehemu nyingine zote za unabii zilizotangulia zilikuwa zimetimia bila swali katika wakati wake uliopangwa.

Wote kwa pamoja walikuwa wakifahamu na kupatana katika orodha hii, usipokuwa tu kwamba halikuonekana tukio lolote la kujibu juu ya kutakaswa kwa patakatifu kulikofanyika mwaka 1844. Kukataa kwamba siku hazikuishia wakati huo kulikuwa ni kuvuruga swala zima, na kupinga misimamo iliyokuwa imejengwa kwa utimizo bayana ya unabii.

Inaendelea tafadhari baki nasi......

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.