Sisi sote tuko chini ya mmoja au mwingine wa manaodha wakuu wawili. Mmoja ni Muumbaji wa mbingu na nchi, ndiye mkuu kuliko wote.
Wote wanatakiwa kumpa utii wa mwili wao wote, kumpa mapenzi yao yote.
Kama akili inakabidhiwa kwake ili itawaliwe, na kama Mungu anahusika kuzibadilisha na kuzikuza nguvu za akili, basi, nguvu mpya za maadili zitapokelewa kila siku kutoka kwa huyo aliye Chimbuko la hekima yote na nguvu zote.
Shetani ndiye nahodha (Kiongozi) wa wale wanaoipenda dunia....
Lengo lake kubwa Sana ni kuwakusanya chini ya bendera yake umati mkubwa sana wa walimwengu, ili idadi kubwa ipate kusimama dhidi ya nguvu ya haki na kweli ya milele. Talanta na nguvu zilizotolewa na Mungu hutumika kwa kazi yake, yaani, huwekwa miguuni pa yule mwasi mkuu wa serikali ya Mungu....
Wakati yule hekima mpenda ulimwengu huu anapita kwa juu juu tu, akiyashika mambo ya kuona tu na kusikia, yule anayemcha na kumheshimu sana Mungu anaufikia umilele, akipenya mahali pa ndani sana na kukusanya maarifa na utajiri ambavyo hudumu milele.
Haki, heshima, upendo, na kweli ndizo sifa za kiti cha enzi cha Mungu.
Hizo ndizo kanuni za serikali yake. . . Hizo ndizo johari za kutafutwa na kutunzwa sana kwa wakati huu na kwa milele. . .
Kutembea ktk ulimwengu huu ukiwa mtu safi mwenye maadili yaliyokuwa na dosari, ukichukua kanuni takatifu za ile kweli ktk moyo wako, mvuto wake ukionekana ktk matendo ya maisha yako;
ukiishi bila kupotelewa na uovu, uongo, na unafiki wa ulimwengu huu ambao utatakaswa hivi karibuni kwa moto wa haki ya upatilizaji wa Mungu kutokana na upotovu wake wa maadili, unatakiwa kuwa mtu ambaye kumbukumbu zako zimewekwa ktk kumbukumbu zile za milele kule mbinguni, ukiwa unaheshimiwa miongoni mwa malaika watakatifu wanaopima na kutathmini kufaa kwa maadili yako. Hiyo ndiyo maana ya kuwa mtu wa Mungu. Letter 41, 1877.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon