JINSI YA KUTUNZA UPENDO NA URAFIKI KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI



Watu Wengi Ambao Wako Kwenye
Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao
Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa
Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao.
Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao
Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua
Taratibu Kama Barafu Iyeyukavyo Juani.
Ili Kuepuka Yote Haya, Hauna Budi
Kujifunza Njia Za Kuwasha Upya Moto Wa
Upendo Kila Wakati Kwa Kuongeza
Ukaribu (Intimacy) Kati Yako Na
Mwenzako.
Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia

1 . KUCHEKA PAMOJA NA
MWENZI WAKO

Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama
Mwaweza Kucheka Pamoja Basi
Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa
Mwaweza Kuaminiana Zaidi Katika
Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza
Kuitofuta Furaha Katika Kila Kitu Basi
Unaweza Kupenya Katika Vyote. Usiwe
Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali Katika
Kila Kitu. Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza
Kuelekea Kwenye Kukasirika Na Badala
Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa
Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi
Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa
Ofisini Na Hata Kwingine Kokote.

2 . KUTIANA MOYO NA
MWENZI WAKO

Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo
Kwa Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na
Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na
Kufuatilia Vile Mwenzako Afanyavyo Au
Apendavyo.
Onyesha Heshima Katika Vitu Hivyo Pia.
Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za
Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu.
Mjenge Mwenzako Mbele Ya wengine Na
Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu
Zimwendee Yeye. Mruhusu Mpenzi Wako
Ajue Kuwa Una Mkubali Katika Kila
Afanyalo. Zaidi Tunavyo Wainua Wapenzi
Wetu Ndivyo Wanavyotuthamini Na
Kutunyanyua Na Sisi Pia.

3 . KUPENDA KUGUSANA
NA MWENZI WAKO

Nguvu Ya Mguso Wa Ukaribu Kamwe
Haiwezi Kulinganishwa Na Chochote.
Lazima Mjifunze Kujenga Tabia Ya
Kugusana Mara Mpatapo Nafasi Sio Tu
Mnapokuwa Mmelala. Kugusana Huku Ni
Pamoja Na Kushikana Mkono Mkiongea Au
Mkitembea, Kukumbatia Bega, Kugusa Au
Kuchezea Nyewele Za Mwenzako Na Njia
Nyingine Zozote Za Kuonyesha Ukaribu
Kimwili. Wengi Wetu Huweza Kufanya
Haya Kidogo Tunapokuwa Peke Yetu Na
Kamwe Sio Mbele Ya Watu, Je, Ni Aibu,
Nidhamu Mbaya? Dhambi?
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha
Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize
Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje
Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye
Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote
Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio
Wapweke.
Mguso Huu Wa Upendo Haumaanishi
Mguso Wa Tendo La Ndoa, Ingawa Pia Ni
Vyema Kujifunza Kuijenga Lugha Ya
Mguso Wa Tendo La Ndoa Katika
Uhusiano Wenu.

4 . ZUNGUMZA HISIA
ZAKO NA ZA MWENZI
WAKO

Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi
Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya
Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa
Majadiliano. Lazima Wapenzi Wajifunze
Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile
Maisha Yasivyo Na Ukamilifu, Uhusiano Na
Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi
Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia
Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na
Umpendaye Jinsi Unavyojisikia Na Nini
Kinachokusumbua. Kuendelea Na
Migogoro Isiyosuluhishwa Husababisha
Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako.
Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa Kutoka Ili
Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie
Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku Na
Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza
Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa
Kuwa Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu
Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka.

5 . MSAMEHE MWENZI
WAKO NA KUBALI
KUSAMEHEWA NAYE

Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu
Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze
Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe
Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano
Kupo Sana, Na Lazima Tuwape
Tuwapendao Nafasi Ya Kuelezea Vile
Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za
Mmoja Wetu Zina Umuhimu. Huwezi
Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako
Akwambie Yanayomuumiza Na
Msameheane.

6 . LINDA MWONEKANO
WA MWENZI WAKO

Mara Nyingi Hatari Hii Hutokea
Tunapokuwa Katika Mizunguko Ya Huku
Na Huko. Ukaribu Na Mpenzi Wako
Hauendelezwi Tu Bali Unalindwa.
Mwonekano Wetu Lazima Uwe Halisi Na
Siyo Bandia . Vile Tunavyoviona Katika
Tamthiliya Na Filamu Siyo Ukaribu Ulio
Halisi. Kama Tunataka Tuonekane Sawa
Na Vile Tunavyowaona Wengine
Wanavyopendana Basi Tunakosea Na
Kujizuia Kuwa Na Mtazamo Bora Katika
Uhusiano Wetu. Ukianza Kupata Ukaribu
Wa Kweli Baina Yako Na Mwenzako,
Utapoteza Hisia Ya Kuhitaji Ukaribu Huo
Na Mwingine Yeyote, Na Badala Yake
Utaanza Kuulinda Ukaribu Mlionao.
Lengo Liwe Kuvitafuta Vile Vyote Mpenzi
Wako Alivyonavyo Ambavyo Ni Kukuza
Ukaribu Wenu. Mwenzako Awe Ndiyo Mtu
Wa Muhimu Kuliko Wote Katika Maisha
Yako.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.