Mungu wetu atatupigania. Nehemia 4:20.
Urejeshwaji wa ulinzi wa Yerusalemu haukusonga mbele bila vizuizi. Shetani alikuwa akifanya kazi kuinua upinzani na kuleta hali ya kukata tamaa… Lakini badala yake, dhihaka na kejeli, upinzani na vitisho, vilionekana kumtia moyo Nehemia kwa dhamira thabiti zaidi na kumuamsha kwa ajili ya kuwa macho zaidi. Yeye alitambua hatari ambazo ni lazima zikabiliwe katika vita hii dhidi ya maadui zake, lakini ujasiri wake haukutishika. Anasema, “Sisi tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi, mchana na usiku.”….
Kando ya Nehemia alisimama mpiga tarumbeta na katika sehemu mbalimbali za ukuta waliwekwa makuhani wakishikilia tarumbeta takatifu. Hawa watu walikuwa wamesambaa katika kazi zao; lakini walipokabiliana na hatari katika hatua yoyote, ishara ilitolewa kwa ajili yao kukarabati pale bila kuchelewa. Nehemia anasema, “Hivyo tukajitia katika kazi hiyo; na nusu yao waliishika mikuki, tangu alfajiri hata nyota zikatokea.”… Nehemia na wenzake hawakunywea kutokana na ugumu na huduma iliyokuwa tata. Mchana na hata usiku, wala hata muda mfupi waliopata kulala, hawakutoa nguo zao, au kuweka silaha zao pembeni.
Upinzani na kukata tamaa ambako wajenzi walikutana nako wakati wa Nehemia kutoka kwa maadui waliokuwa wazi na waliojidai kuwa marafiki ni uzoefu dhahiri ambao wale wanaomfanyia Mungu kazi watakutana nao. Wakristo hujaribiwa, siyo kwa hasira tu, dharau na ukatili wa maadui, bali pia uzembe, hali ya ukinzani na kutofuata taratibu, uvuguvugu na hila za wale wanaosema kuwa ni marafiki na wasaidizi wetu…
Shetani anatumia nafasi ya kila sehemu ambayo haikuwekwa wakfu kwa ajili ya kukamilisha makusudi yake. Kati ya wale wanaodai kuwa waunga mkono wa kazi ya Mungu, wapo wale ambao huungana na maadui wake na hivyo kufungua milango kwa mashambulizi ya maadui zake wabaya zaidi dhidi ya kazi yake. Hata baadhi ya wale wanaotamani kazi ya Mungu ifanikiwe, wao pia watadhoofisha mikono ya watumishi wake kwa kusikiliza, kutoa taarifa, na kuamini nusu uzushi, majivuno na vitisho vya maadui wake…. Mwitikio wa imani leo utakuwa ule uliofanywa na Nehemia, “Mungu wetu atatupigania;” kwani Mungu yumo kazini na hakuna mtu awezaye kuzuia mafanikio yake hatimaye.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon