Na baada yao wakafanyiza Watekoi; lakini wakuu wao hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao. Nehemia 3:5.
Kati ya wale waliokuwa wa kwanza kushika roho ya ari na bidii ya Nehemia walikuwa makuhani. Kwa sababu ya nafasi yao yenye mvuto, watu hawa wangeweza kufanya mengi katika kuiendeleza kazi au kuizuia na hali yao ya kuwa tayari kushirikiana katika hatua ya mwanzo kabisa, ilichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio yake. Wengi kati ya wakuu na watawala wa Israeli walijitokeza kiungwana kwa ajili ya jukumu lao na hawa watu waaminifu wanatajwa kwa heshima kwenye kitabu cha Mungu. Walikuwepo wachache, Watekoi, ambao “hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao.” Kumbukumbu ya watumishi hawa wazembe imewekwa kama alama ya aibu na imekabidhiwa katika vizazi tangu wakati huo kama onyo kwa ajili ya vizazi vyote vilivyokuwa vije baadaye.
Katika kila vuguvugu la kidini wapo baadhi ya watu ambao, japo hawakatai kwamba kazi ni ya Mungu, huwa wanaendelea kujitenga, wakikataa kufanya jitihada yoyote ya kushiriki. Ingekuwa bora kwa watu wa namna hiyo kukumbuka juu ya rekodi inayotunzwa mbinguni – kile kitabu ambacho hakiwezi kufutwa, kisicho na makosa na ambacho kutokana nacho watahukumiwa. Pale, kila fursa iliyopuuziwa ya kutumika kwa ajili ya Mungu, imerekodiwa; na pale pia, kila tendo la imani na upendo limewekwa katika kumbukumbu ya milele.
Ukilinganisha na mvuto uliotia moyo wa kuwepo kwa Nehemia, mfano wa waungwana wa Tekoi haukuwa na uzito. Kwa ujumla, watu walikuwa wamehamasika kutokana na uzalendo na ari. Watu wenye uwezo na mvuto waliwapanga raia mbalimbali katika makundi, kila kiongozi akiwajibika kwa ajili ya kujenga sehemu fulani ya ukuta. Kwa ajili ya baaadhi ya hawa imeandikwa kwamba walijenga, “kila mtu kuielekea nyumba yake.”
Kwa vile kazi ilikuwa imeanza hakika, nguvu za Nehemia hazikupungua. Huku akiwa macho bila kuchoka, alisimamia ujenzi, akiongoza wafanyakazi, akitambua vizuizi na akishughulikia dharura… Katika shughuli zake nyingi, Nehemia hakusahau chanzo cha nguvu zake. Moyo wake ulidumu kuinuliwa kwa Mungu, yeye aliyemsimamizi wa wote. Yeye alisema, “Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha;” na maneno haya, huku yakirudiwa rudiwa kama mwangwi, yalifurahisha mioyo ya wafanyakazi wote kwenye ukuta.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon