Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Zekaria 4:10.
Katika kujenga tena nyumba ya Bwana, Zerubabeli alifanya kazi akikabiliana na matatizo mengi ya namna mbalimbali. Tangu mwanzo, maadui wanatajwa hivi “wakaidhoofisha mikono ya watu wa Yuda, wakawasumbua, walipokuwa wakijenga,” “wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.” Lakini Bwana aliingilia kwa niaba ya wajenzi na sasa akanena kupitia kwa nabii wake Zerubabeli akisema, “Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare.”…
Katika historia yote ya watu wa Mungu, milima mikubwa ya matatizo, inayoonekana kutoondoleka, imeonekana kusimama kwa namna ya kutisha mbele za wale waliojaribu kukamilisha makusudi ya Mbingu. Vikwazo kama hivyo huwa vinaruhusiwa na Bwana kama jaribio la imani. Tunapokuwa tumezungukwa kila mahali, huu ndio wakati wa kumtumainia Mungu na katika nguvu ya Roho wake, kuliko wakati mwingine wowote. Zoezi la imani iliyo hai linamaanisha ongezeko la nguvu ya kiroho na maendeleo ya imani isiyoyumba. Ni kwa namna hiyo, ambapo nafsi inakuwa nguvu inayoshinda. Vikwazo vinavyowekwa na Shetani kwenye njia ya Mkristo vitatoweka mbele za masharti ya imani; kwani nguvu za mbinguni zitakuja kumsaidia. “Wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.”
Njia ya kidunia huwa inaanza kwa majigambo na majivuno. Njia ya Mungu huwa inafanya siku ya mambo madogo kuwa mwanzo wa mafanikio makubwa ya ukweli na uadilifu. Nyakati fulani Mungu huwa anafundisha watendakazi wake kwa kuwaletea hali za kuvunjika moyo na mwonekano wa kushindwa. Ni kusudi lake kwamba watu wake wajifunze kuyadhibiti matatizo.
Mara kwa mara watu huwa wanajaribika kusita mbele za fadhaa na vikwazo vinavyowakabili. Lakini kama watashikilia mwanzo wa tumaini lao kwa uthabiti hadi mwisho, Mungu atafanya njia iwe dhahiri… Mbele za roho ya ujasiri na imani isiyoyumba ya Zerubabeli, milima mikubwa ya matatizo itafanywa kuwa tambarare; naye ambaye mikono yake imeweka msingi, “mikono yake ndiyo itakayoimaliza.”
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon