MOTO WA KIGENI NDANI YA VAZI LA UKRISTO.



Kisa cha Ahazi mfalme juu ya kutumaini waganga kinapatika katika kitabu cha 2 Wafalme 1:1-18. 

Ahazia "akaanguka katika dirisha la chumba chake," na kuumia vibaya sana. Akaogopa mambo yatakayotokea kwa ajili ya kuanguka huko, alituma baadhi ya watumishi wake ili kuulizia kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba atapona au la. Ilidhaniwa kwamba mungu wa ekroni atatoa jawabu, kwa njia ya makuhani wake. Kwamba anaweza kubashiri mambo ya mbele. Watu wengi walikuwa wakienda kuulizia habari; lakini majawabu yaliyopatikana na maelezo yote yalikuwa yakitoka kwa mungu wa giza - Ibilisi.

Watumishi wa Ahazia walikutana na mtu wa Mungu, ambaye aliwarudisha kwa Mfalme, wakiwa na Ujumbe mkuu: "Je, ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu mungu wa Ekroni? Basi sasa, Bwana asema hivi: Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa."
Nabii alipomaliza kutoa Ujumbe wake aliondoka.

Watumishi walirudi kwa haraka na kwa mshangao mpaka kwa Mfalme, wakamkariria maneno ya mtu wa Mungu. Mfalme aliwauliza: "Alikuwa mtu wa namna gani? Nao wakamjibu: " Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema: ndiye yule Eliya Mtishibi." Alijua kuwa kama ni Eliya aliyekutana na watumishi wake, na kuwambia maneno yale, hakika yatatimia. Akiwa na wasiwasi sana, na akijaribu kuepusha adhabu hiyo asitimizwe, alituma watu kumwita nabii.

Ahazia alituma askari akijaribu kumtisha Eliya, na mara mbili walipata adhabu kutoka kwa MUNGU. Kikosi cha tatu cha askari kilijinyenyekeza mbele ya Mungu, na mkuu wao alipomkaribia Eliya, "akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako."

"Malaika wa Bwana akamwabia Eliya, shuka pamoja naye, usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa Mfalme.
Akamwambia, Bwana asema hivi: Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, je, ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa." Ahazia alishuhudia matendo makuu ya Mungu wakati wa utawala wa Baba yake. Alikuwa ameona ushuhuda wa kutisha, kuhusu Waisrael waasi, jinsi Mungu alivyowatendea wale walioidharau sheria yake.
Mambo ya kutisha yote hayo, kwa Ahazia yalikuwa kama mchezo tu.
Badala ya kujinyenyekeza mbele za Bwana, alifuata Baali, kitendo ambacho kilionyesha ukaidi wake mkuu. Ahazia alikufa katika hali hiyo ya uasi, bila kutubu, "sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya."

Habari ya dhambi za Mfalme Ahazia na adhabu aliyopata, hutoa maonyo kwa wote kwamba, hakuna mchezo kwa kuasi bila hofu.
Wanadamu leo wanaweza wakawa hawaheshimu miungu ya mataifa, walakini watu maelfu huabudu katika mahekalu ya Shetani kama alivyofanya Mfalme wa Israeli.

Roho ya kuabudu sanamu imeenea ulimwenguni kote leo, ingawaje kwa ajili ya elimu na sayansi, inaonekana tofauti kidogo na jinsi ilivyokuwa wakati Ahazia alipokwenda kuuliza kwa mungu wa Ekroni. Kila siku ipitayo huzuni huongezeka kwa vile inavyoonekana kwa watu kutojali neno la unabii lililo imara; ila badala yake hufuata madanganyo ya Kishetani, yaani elimu ya uongo.

Leo siri ya ibada ya sanamu ya kimataifa imeachwa, na badala yake zinafuatwa njia za kushirikisha mambo ya siri na maajabu ya kiroho ambayo huongozwa na Shetani. Mafunuo haya ya kiajabu - ajabu hukubaliwa na watu maelfu ambao hukataa kufuata nuru ya neno la Mungu, au maongozi ya Roho wake. Watu hawa wenye kuamini roho za kiajabu - ajabu wanaweza kuwacheka wanajimu na wenye roho za uaguzi wa zamani; lakini mdanganyaji mkuu huwacheka tu na kushangilia kwa vile wanavyokubali kufuata madanganyo yake, ingawa ni kwa umbo jingine kuliko zamani.

Wako watu wengi wasiotaka kuongozwa na roho ya uaguzi, lakini roho ile ile inapokuja kwa umbo jingine huwa tayari kuifuata.
Wengine hupotoshwa na mafundisho ya sayansi ya Kikristo na mafundisho ya dini ya namna nyingine nyingine.

Wajumbe wa dini hizi za roho hujidai kuwa wanao uwezo wa kuponya. Husema kuwa uwezo huo umo katika mawazo ya mtu, nao hufanya kazi kwa namna ya nguvu za umeme na sumaku, nao huuita, "dawa ya huruma." Sio watu wachache wanaofuata waponyaji hawa, badala ya kumwendea na kumtumaini Mungu aliye hai na waganga halisi waliofundishwa uganga barabara.

Mama mtoto, anayemwangalia mtoto wake aliye katika hali ya kufa, husema: "Sina la kufanya. Je, hakuna mganga mwenye uwezo wa kumponya mwanangu?" Ndipo anapoambiwa habari za mponyaji wa ajabu anayeponya watu kwa miujiza, naye hutumainia mganga wa jinsi hiyo, na kumkabidhi mtoto wake mikononi mwa mtu kama huyo, ambaye kwa kweli ni kama kumkabidhi kwa Shetani hasa. Kuna mifano mingi ya mambo ya jinsi hii, ambayo inathibitisha kwamba, hali ya baadae ya mtoto kama huyo huwa ikitawaliwa na uwezo wa Shetani, ambavyo huwa vigumu kuvunja hali hiyo.

Mungu alikuwa sababu ya kutopendezwa na ukaidi wa Ahazia.
Tangu mwanzo ameonyesha kwamba, "furaha yake ilikuwa pamoja na wanadamu." Mithali 8:31.
Yeye amekuwa msaada ulio karibu sana kwa watu wote waliomwita kwa uelekevu wa moyo. Na kutafuta msaada kwa miungu ya mataifa, ambayo ni adui wa Mungu, anawatangazia wote kuwa, anaiamini miungu zaidi ya anavyomwamini Mungu wa mbinguni. Kwa njia hiyo hiyo watu umdharau Mungu, wanapogeukia kwa uwezo wa giza. Je, Ikiwa kitendo cha Ahazia kilimkasirisha, itakuwaje kwa watu wanaojua ukweli halisi halafu wanachagua kuenenda gizani pia?

Wale wanaokubali kufuata uchawi wa Shetani, wanaweza kudhani kuwa wamepata mafanikio makubwa; lakini Je, wakiwa katika hali hiyo wako salama, au uchaguzi wao huo ni wa busara? Je, kama maisha yakirefushwa, itakuwaje? Je, kama wakifanikiwa kwa muda kitambo, mwishoni itawafaa kama wakidharau mapenzi ya Mungu?
Faida na mapato yote ya namna hiyo, mwisho yataonekana kuwa ni hasara tupu. Hatuwezi kuvunja uzio ambao Mungu aliuweka kutulinda na uwezo wa Shetani kukaidi bila kupata hasara.
(Manabii na Wafalme, uk. 106-108)

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.